Sunday

ALICHOSEMA HASA PROF. LIPUMBA MSIKITINI JUZI NA KUJIKANYAGA KANYAGA!!

      

Zimbabwe yapiga kura ya maoni ya katiba

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekanusha malalamiko kwamba wananchi hawakuelezewa ipasavyo kuhusu katiba mpya.

Bwana Mugabe aliiambia BBC kwamba Wazimbabwe walishauriwa sana kuhusu katiba hiyo na walitoa maoni yao.

Kura ya maoni kuhusu katiba mpya inafanywa nchini Zimbabwe leo.

Chama cha Rais Mugabe cha Zanu-PF na kile cha MDC cha Morgan Tsvangirai ambacho kimo kwenye serikali ya mseto, vinaunga mkono katiba mpya.

Waandishi wa habari wanasema wakati wa kampeni pamekuwa na mvutano nchini Zimbabwe kabla ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanywa baadae mwaka huu.

Vyama vikuu vya Zimbabwe vina msimamo mmoja kuhusu katiba inayopendekezwa.
Vinaiunga mkono.

Inavoelekea katiba itakubaliwa na wengi lakini inawezekana wataojitokeza kupiga kura ya maoni ni wachache.
Katiba hiyo ni muhimu kuielekeza nchi kwenye uchaguzi huru na wa haki.
Ina vipengee vya haki za wananchi na vizuizi dhidi ya madaraka ya rais mtendaji.
La kutatanisha ni kuwa katiba mpya inataka rais atumike kwa mihula miwili ambayo itampa Rais Mugabe, mwenye umri wa miaka 89, uwezekano wa kuongoza kwa miaka kumi zaidi

PAPA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI

Papa Francis aliyechaguliwa hivi karibuni, amekutana na waandishi wa habari mjini Rome akisema kuwa atapenda kanisa maskini lenye lengo la kuwasaidia maskini.
Katika hatua ambayo Vatikani imesema inaonesha uwazi zaidi, Papa mpya alizungumza na mamia ya waandishi wa habari na alisema alichagua jina la Mtakatifu Francis wa Assisi kwa sababu alikuwa mtakatifu wa amani, matumizi haba na kutumikia maskini

"Wakati wa uchaguzi wa papa mpya kando yangu alikuwa Askofu wa Sao Paulo, Claudio Hummes.

Ukweli ulipokuwa unakaraibia alinipoza.

Na kura zilipotimia thuluthi mbili alinikumbatia na kunibusu.

Aliniambia "usiwasahau masikini".

Na hilo limebaki nami...masikini, masikini

Saturday

MITANDAO YACHANGIA ONGEZEKO LA KASI YA UKAHABA VYUONI (UDSM) (UDOM) (CBE) (IFM)(SAUTI)


 Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo. Imefahamika kuwa Baadhi ya wanafunzi wanatumia mitandao ya kijamii katika kufanikisha biashara ya ngono. PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi.
Uchunguzi umebaini kuwa matumizi mabaya ya teknolojia hasa mitandao ya kijamii yamechochea ongezeko la uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya na zaidi biashara ya ukahaba vyuoni.
Mitandao ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa namna inavyoweza kuwaunganisha watu kutokana na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga mitandao ya kibishara, kidini, michezo, burudani, vichekesho na mengine ambayo mara nyingi huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na kuona kinachoendelea ndani.
Mbali na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi yanayoendesha biashara ya ukahaba, yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini kwa kupitia kurasa mbalimbali kama vile ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyinginezo.

Uchunguzi umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kutumia mitandao wameweka picha na namba kwa ajili ya mawasiliano kwa mteja atakayekubaliana na bei waliyoweka.

Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia katika mitandao ya Facebook, Twitter, BBM, Instagram, utabaini kuwapo kwa makundi yaliyoundwa kutengeneza mitandao ya ngono, ambayo huweka pia namba za simu za wahusika, zikiambatana na picha, ambao ikiwa utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza ukapiga simu husika kuzungumza naye kwa kufanya mapatano kabla ya kukubaliana.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao hiyo. 
Baadhi ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na kujitangaza kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Kwa nyakati tofauti, waandishi wa gazeti la Mwananchi walitembelea makundi yanayojinadi kufanya biashara hiyo pamoja na kufanya mawasiliano na wasichana watatu ambao waliweka picha na namba zao kwenye mtandao

Monday

Uhuru Kenyatta ndiye rais tajiri zaidi barani Afrika

On Streets Today

Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta ndio rais tajiri zaidi barani Afrika. Kenyatta alikamata nafasi ya 26 mwaka 2011 kwenye orodha ya watu matajiri zaidi barani Afrika kwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 500.
Mtoto huyo wa rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta nimrithi wa mali kibao zilizopo Kenya. Anamiliki ardhi yenye ukubwa wa acre 500,000 katika maeneo mbalimbali nchini humo. Ardhi hiyo ilikuwa ya baba yake aliyoipata miaka ya 1960s na 1970s baada ya serikali ya kikoloni ya Uingereza na benki ya dunia kuwezesha maofisa wa serikali wa Kenya na matajiri kupata ardhi kutoka kwa waingereza kwa bei chee.
Uhuru na familia yake wanamiliki kampuni ya Brookside Dairies ambayo ni kubwa zaidi nchini Kenya kwa utengenezaji wa maziwa na pia ana hisa nyingi kwenye kituo cha TV cha K24 pamoja na benki moja kubwa ya biashara jijini Nairobi. Pia ana miradi mingine kibao.

PICHA ZA UCHI ZA MSANII SAPNA WA STEVE R & B ZANASWA

On Streets TodayWAKATI mabinti wengi hasa mastaa wa Bongo wakijuta baada ya picha zao za utupu walizopigwa na wapenzi wao kuvuja, kwa msanii mrembo aliyepamba video ya wimbo wa Bongo Fleva uitwao Jambojambo wa msanii Steve R&B,Aisha Firozi ‘Sapna’ ni kawaida kwani hujifotoa mwenyewe.


Chanzo makini cha Risasi kimewasilisha folda lenye picha za kutosha za mrembo huyo akiwa mtupu huku kikieleza kwamba ni mchezo wake kujipiga mwenyewe picha hizo.


Kwa sharti la kutochorwa jina lake , chanzo hicho ambacho kipo aribu na Sapna kilisema:“Yule ni mtu wangu wa karibu sana, lakini tabia yake kwa kweli huwa siipendi kabisa. Anajipiga picha chafu mwenyewe, kwake ni starehe kubwa, huwezi kuamini.”

Kikiendelea ufunguka zaidi, chanzo hicho kilipasha kuwa, picha hizo amejipiga hivi karibuni nyumbani kwa rafiki yake aitwaye Doreen, Tabata - Magengeni jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa akiishi naye.

KAULI YA SAPNA.....Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni; Sapna alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu kunaswa kwa picha hizo, kwanza alishangaa lakini akakiri kuzitambua.
“Hizo kweli ni picha zangu na nilijipiga mwenyewe sasa sijui wewe umezipataje na zimefi kaje huko kwenu? Mimi nilipiga kwa masilahi yangu mwenyewe, huwa natamani sana kujiangalia jinsi umbo langu lilivyo, ndiyo maana niliamua kujipiga na si vinginevyo.
“Kila mtu na maisha yake na mimi sikuwa na dhamira mbaya kujipiga picha hizo zaidi ya kujiangalia tu nilivyo,” alisema Sapna.

TID APEWA KICHAPO KIKALI NA MTANGAZAJI WA CLOUDS TV

On Streets Today


Mwanamuziki nyota wa Bongo flava ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki wa dansi, Khalid Mohammed ‘TID’, wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya kudundwa hadi kutolewa nundu puani na mtangazaji wa Clouds TV, Cedou Ayoub a.k.a Babuu.
Tukio hilo la aina yake lililotokeawiki iliyopita kwenye kiota cha burudani Bongo pale Club Maisha na kushuhudiwa na watu kibao ambapo chanzo chake kikidaiwa ni kudaiana hela.
Chanzo chetu kilimwaga umbea kuwa, siku ya tukio hilo TID alikuwa amealikwa kwenye uzinduzi wa albamu ya mwanamuziki Country Boy iliyokuwa inafanyika mjengoni humo, ambapo baada ya onesho hilo kuisha ndipo TID akiwa ‘mitungi’ alimfuata Babuu na kuanza ‘kumzingua’.
Hata hivyo, chanzo chetu kiliendelea kueleza kuwa, baada ya walinzi wa ukumbi huo kuona hali tete ya uvunjifu wa amani waliwasihi watu hao kutoka nje kabisa ya ukumbi, huku mtangazaji huyo akiwaomba walinzi hao wawaache wapimane ubavu kidogo na walipotoka nje wakaachiwa ‘ulingo’ ndipo ngumi zilianza kupigwa.
Habari zaidi toka eneo la tukio zilisema kuwa: “Watu waliwazunguka huku wakishangilia kwa muda wa dakika tano ngumi zinapigwa ndipo maabaunsa wakawaamua, lakini, tayari TID alikuwa ameshatolewa manundu kadhaa puani.”
Aidha, kwa upande wa Babuu, alipotafutwa kupitia simu yake ya kiganjani, iliita bila kupokelewa.

Hata hivyo, watu wa karibu na Babuu walilieleza gazeti hili kuwa, kufuatia TID kuchezea mkong’oto huo, kumezuka ‘bifu’ kubwa na kuna wasiwasi wa kutekana kwa mastaa hao hivyo huku Mkurugenzi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba akitakiwa kuingilia kati suala hilo ili kuepusha balaa.

BOFYA HAPA ILI KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012

On Streets Today

http://www.necta.go.tz/matokeo2012/csee2012/olevel.htm

Sunday

ALICHOANDIKA MH ZITTO KABWE BAADA YA KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA MASHIKA YA UMMA KUFUTWA NI HIKI. @ZittoKabwe


On Streets Today

Katika mkutano wa Kumi wa Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Spika wa Bunge ndugu Anna Makinda alitangaza mabadiliko kadhaa ya muundo wa Bunge katika Kamati mbalimbali za Bunge. Moja ya maamuzi ya Spika yalikuwa ni kufutwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ambayo inajulikana kifupi kama POAC.

Maamuzi haya yameleta sintofahamu kwa wananchi wengi na wafuatiliaji wa masuala ya Bunge na Uwajibikaji katika nchi yetu. Ni muhimu tufahamu uundwaji wa POAC ulitokana na misingi gani na kwamba Uamuzi wa Spika unarudisha nyuma maendeleo makubwa ya kujenga Bunge imara na lenye meno. Maamuzi ya Spika ni kinyume cha kanuni za Bunge, sheria ya Ukaguzi na Katiba ya nchi. Maamuzi ya Spika yanavuruga Bunge,ni ya hovyo na yanapaswa kupingwa na kila mdau wa Uwajibikaji nchini.

Baada ya Tanzania kuingia kwenye zoezi la Ubinafsishaji, mashirika mengi ya Umma yaliuzwa na mengine kufa kabisa. Wakati huo kulikuwa na chombo kinaitwa SCOPO (Standing Committee on Parastatal Organisations) kwa madhumuni ya kusimamia uendeshaji wa Mashirika ya Umma. Bunge lilikuwa na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma na kamati hiyo ilifutwa mwaka 1997 kufuatia hatua za ubanifsishaji na ukweli kwamba Mashirika ya Umma hayatakuwapo na hivyo hapakuwa na haja ya kuwapo kwa kamati hiyo. Mwenyekiti wa mwisho wa Kamati hiyo alikuwa ni Mzee William Shellukindo wakati huo akiwa Mbunge wa Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga.


.

Mwaka 2007, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alifanya mkutano wa Uwajibikaji na kueleza Taifa kuwa kimsingi Mashirika ya Umma bado yapo na mahesabu yao, kwa kuwa hayaangaliwi, ni mabaya sana nafedha za umma zinapotea. Pia alieleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 143(5) inamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoa taarifa za Ukaguzi za Mashirika ya Umma (Public Authorities and Other Bodies). Hivyo aliomba Bunge liunde Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ili liweze kupokea, kujadili na kutoa maelekezo kuhusu mahesabu ya Mashirika ya Umma na kusimamia ufanisi wa Mashirika ya Umma. Vile vile alishauri Kamati hiyo isimamie sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma. Spika wa Bunge wa wakati huo, kupitia Kamati aliyoiunda chini ya Job Ndugai (wajumbe wengine walikuwa dkt Willibrod Slaa, Beatrice Shelukindo, Hamad Rashid Mohammed na Nimrod Mkono) wakaunda Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma kwa mujibu wa Kanuni za Bunge za Mwaka 2007. Kamati ya POAC iliundwa rasmi mwaka 2008 mwezi Februari. Nilipewa dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kamati hii. Sababu za kuanzishwa kwa kamati ya POAC bado zipo na kimsingi sababu hizo ni za maana sana sasa kuliko ilivyokuwa kabla.

Majukumu ya POAC yaliainishwa na sehemu ya tatu ya nyongeza ya nane ya Kanuni za Bunge toleo la mwaka 2007, kanuni ya 115 (13)(a-e). Majukumu hayo ni pamoja na kushughulikia mahesabu yaliyokaguliwa ya Mashirika ya Umma, kuainisha maeneo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za Umma, kutathmini ufanisi wa Mashirika ya Umma na kufuatilia utekelezwaji wa sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya Umma. Kuanzia mwaka 2008 Mdhibiti na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali amekuwa akitoa taarifa za mahesabu ya mashirika kama Katiba ya nchi inavyomtaka na sheria ya ukaguzi ya mwaka 2008. Sheria hii imeitaja kamati ya POAC kama moja ya kamati zenye majukumu ya kuwasilisha Bungeni taarifa ya mwaka ya mahesabu ya Mashirika ya Umma.

Katika kipindi cha miaka mitano POAC imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa umahiri na kwa kweli kwa uwazi sana kuliko kamati nyingine zote za Bunge. Taarifa ya mwisho ya POAC katika Bunge iliyowasilishwa katika mkutano wa saba wa Bunge, mwezi Aprili mwaka 2012 ulipelekea kutolewa kwa hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ambayo ilisababisha mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri. Hatua hii ilikuwa ni hatua muhimu sana katika kuweka mizizi ya utamaduni wa uwajibikaji nchini kwetu. Wakati Kamati inajiandaa na Taarifa yake ya Mwaka 2012 kwenye Mkutano wa Kumi na Moja, Spika ameivunja. Ikumbukwe maagizo ya mwisho ya Kamati ya POAC yalikuwa ni kuzuia mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa mikopo kwa Serikali bila ya kuwapo kwa mikataba. Hivi sasa Serikali imekopa zaidi ya shilingi 1.2 trilioni kutoka mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa ajili ya miradi mbalimbali, mikopo hiyo ya fedha za wafanyakazi haina mikataba yeyote na POAC iliona hatari ya fedha za wafanyakazi kupotea na kuleta madhara makubwa kwa wastaafu nchini.


.

Katika maelezo yake Spika amesema nchi nyingine duniani hazina kamati kama ya POAC. Nadhani waliomshauri Spika waliamua kumdanganya na yeye akadanganyika. Nchi zote za Afrika Mashariki zina Kamati ya kusimamia Mashirika ya Umma. Kenya inaitwa Public Investments Committee, Uganda inaitwa State Corporations Committee na hata nchi nyingine kama India ambazo zinafuata utamaduni wa kibunge kama wetu wanayo na wanaita Public undertakings Committee. Nchini Afrika Kusini sio tu kuna Kamati ya Mashirika ya Umma bali pia kuna Wizara inayosimamia Mashirika ya Umma (Ministry of Public Entreprises). Kimsingi Kamati ya POAC ilipaswa kuongezewa nguvu zaidi ili kufikia uwezekaji wa Serikali kwenye makampuni binafsi badala ya kuifuta. Uwezekaji wa Serikali kwenye makampuni kama BP, AirTel, Kilombero Sugar, SonGas nk hauna uangalizi wowote.

Uamuzi wa Spika wa Bunge kuifuta Kamati ya POAC ni uamuzi unaorudisha nyuma juhudi za nchi kujenga asasi za uwajibikaji, ni kinyume cha sheria ya ukaguzi wa umma inayotaja Kamati tatu za Bunge za kusimamia fedha za Umma na ni kinyume cha Katiba ya nchi. Spika wa Bunge anasema kazi za Kamati ya POAC zitafanywa na Kamati ya PAC; Tanzania ina jumla ya Mashirika ya Umma 258 yenye thamani ya shilingi trilioni 10.2 mpaka mwezi Juni mwaka 2012, hata kamati ya POAC ilikuwa haiwezi kushughulikia Mashirika yote ya Umma katika mwaka mmoja, PAC itawezaje kusimamia Wizara za Serikali, Mikoa na wakala za Serikali na wakati huo huo Mashirika ya Umma 258? Kwa vyovyote vile Taifa linarudi miaka ya kabla ya 2008 ambapo Mashirika ya Umma yalikuwa kichaka cha kuiba fedha za Umma. Hivi karibuni Kamati ya POAC iligundua mtindo wa Wizara za Serikali kupeleka fedha Serikali kwenye Mashirika na kutumia kifisadi ili kukwepa ukaguzi kwenye Wizara (Wizara ya Utalii ilipeleka zaidi ya shilingi 600 milioni Bodi ya Utalii mwaka 2010/2011). Ikumbukwe pia wizi wa EPA, MEREMETA na hata uuzaji holela wa baadhi ya mali za Serikali kupitia ubinafsishaji ulifanyika nyakati ambazo Bunge halina kamati inayosimamia Mashirika ya Umma.

Kwa vyovyote vile Spika wa Bunge amedhihirisha namna ambavyo anafanya maamuzi bila kuzingatia maslahi ya nchi wala kuzingatia historia ya uwajibikaji katika nchi. Namna mijadala ya Bunge inavyoendeshwa, namna anavyobeba ajenda za Serikali katika kujenga Bunge kibogoyo na namna anavyofanya maamuzi kwa kukurupuka, inahitaji hatua za kuokoa misingi ya uwajibikaji wa nchi. Ni lazima Spika wa Bunge adhibitiwe kwa kuondolewa katika nafasi hiyo haraka iwezekanavyo. Spika lazima ajue kwamba Mamlaka yapo kwa wananchi na yeye ni msimamizi tu wa vikao vya Baraza la wananchi liitwalo Bunge. Anna Makinda lazima adhibitiwe, vinginevyo nchi yetu itaumia.

PICHA ZA MAGARI 10 ALIYOWAHI KUONEKANA NAYO MWIMBAJI CHRIS BROWN

On Streets Today














Hii ni stori nyingine



KAMA UNAPENDA KUONA VIDEO ZA MUZIKI ZA NCHI NYINGINE AFRIKA, HII POST NI YAKO

On Streets Today













Monday

BREAKING NEWS: PICHA 8 ZA LULU MAHAKAMANI LEO JAN 28 PAMOJA NA MAELEZO YA MASHARTI YA DHAMANA YAKE.

On Streets Today


Lulu akiwa anaingia Mahakamani leo january 28 2013 akiwa na shauku ya kupata dhamana.

Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.

Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.

Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.


.


.


.


.


Hapa ni wakati alipocheka sana pale mwandishi mmoja wa kike ambae pia alikua akimpiga picha alipokua akimlainisha Lulu kwa maneno baada ya mwigizaji huyo kuficha uso wake alipokua akipigwa picha, alisema alikua anaumizwa macho na mwanga wa kamera.


.


.


Mama mzazi wa Lulu ni mwenye nguo nyeupe na nyeusi.

Search This Blog