Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakisalimiana na mchezaji soka nyota wa Uingereza anayechezea Los angeles Galaxy ya Marekani, David Beckham, walipokutana uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London Jumatano, muda mfupi kabla ya Rais Kikwete na Mama Salma kuelekea Washington DC kuhudhuria mkutano wa G8 kwa mwaliko wa Rais Barak Obama wa Marekani. Bekham ameonesha nia ya kutembelea Tanzania kama mtalii siku za karibuni na Rais Kikwete amemkaribisha kwa mikono miwili, akimhakikishia kwamba licha ya kuwa na mashabiki wengi ambao watafurahi kumuona pia atafurahia vivutio kibao vya kitalii.
| Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor |
Rais wa zamani wa Liberia
Charles Taylor anayetuhumiwa kwa makosa ya kivita amewashambulia
waendesha mashtaka kuwa waliwalipa mashahidi wa upande wa mashtaka ili
wamkandamize.
Taylor ambaye alikutwa na hatia mwezi uliopita
alisema hayo wakati akitoa maelezo kwenye mahakama ya Kimataifa ya
makosa ya Jinai ya The Hague.Hiyo ni nafasi yake ya mwisho ya kujieleza katika mahakama hiyo kabla ya kusomewa hukumu baadae mwezi huu.
Taylor alipatikana na hatia ya kuwasaidia waasi nchini Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo pia anaelezwa alisaidia kuendesha mipango ya mauji.
Akitoa maelezo yake Taylor amesema fedha imechukua nafasi katika kesi yake.
"Mashahidi wamelipwa , wamelazimishwa na kwa wakati fulani walitishiwa na waendesha mashtaka kama wasingetoa ushahidi unaonikandamiza", alisema.
Amesema yeye mara zote alikuwa akilaani maauaji popote duniani na aliwahurumia waathirika wa mauaji hayo.
Nje ya mahakama Taylor mara zote amekuwa akipinga makosa yote 11 yanayomkabili huku akisisitiza kuwa hana hatia yoyote.
















