Sunday

STREET NA MATUKIO





STAA wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu na kichwa kinachotingisha katika Bongo Fleva, Nasib Abdul Juma ‘Diamond’ wamenaswa wakiwa beneti mkoani Kigoma.

Chanzo kilichopo mkoani humo, kimepenyeza habari hiyo juzi, ambapo kilisema ukaribu wao uliamsha hisia kwamba huenda wawili hao wamerudiana.

“Wapo wote huku Kigoma, kwa Diamond ni sawa maana yupo na wasanii wenzake wa Kigoma All Stars, sasa Wema amekujaje? Kwanza siyo mwanamuziki, lakini pia siyo mtu wa Kigoma ni wa kutoka Tabora,” kilieleza chanzo hicho.

Baada ya kupata habari hiyo, Ijumaa lilimvutia waya Diamond zaidi ya mara tatu lakini simu iliita bila kupokelewa.

Wema alipopigiwa simu alipatikana na kufafanua ishu nzima ilivyo. Huyu hapa msikie: “Ni kweli nipo huku Kigoma lakini sipo na Diamond. Nimekuja kwa mwaliko wa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini).

“Mimi na Diamond ni marafiki tu, hatuwezi kuwa wapenzi tena, kila mtu na maisha yake. Kifupi nina mtu wangu ambaye tunapendana na kuheshimiana sana.”

Alipotakiwa kumtaja mpenzi wake mpya alisema: “Kwa sasa siwezi kumtaja, lakini siku si nyingi nitamuweka hadharani watu wamjue.”

HATIMAE MTOTO WA KAMBO WA USHER RAYMOND AFARIKI DUNIA


Kyle Glover ambae ni mtoto wa mke wa zamani wa Mwimbaji Usher Raymond, amefariki dunia leo kutokana na kuumia kwenye ajali ya pikipiki za kwenye maji maarufu kama Jetski mwanzoni mwa mwezi huu huko Georgia Marekani.
Madaktari wametoa mashine zilizokua zinasaidia kumuweka hai mtoto huyo aliekua na umri wa miaka 11 baada ya kugundua kwamba majeraha aliyoyapata yasingeweza kutibika.
Kyle akiwa na rafiki yake wa kike mwenye umri wa miaka 15 walipata ajali july 8 2012 huko Georgia baada ya Inner tube waliyokuwemo iliyokua ikivutwa na boti kugongwa na Jetski wakiwa kwenye maji na hivyo kupata majeraha ya kichwa.

NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOFIKA KUMTEMBELEA KAJALA GEREZANI


Pichani ni washkaji zake Kajala walioenda kumtembelea mida hii pale gereza la Segerea na kuanzia kushoto ni Producer Lamar, Producer P.Funk Majani mbele yake ni Shilole msanii wa Bongo Fleva na anayefuatia ni B12 kutoka Clouds FM, VJ Penny, Sam Misago kutoka EATV na meneja wa Ommy Dimpozi anaitwa Muba.

HIKI NDICHO ALICHOKIZUNGUMZA DIAMOND KUHUSU KUTO0KUELEWANA NA BABA YAKE MZAZI NA KAULI ALIYOITOA TID JUU YAKE


Baada y amagazeti kuandika juu ya kutokuelewana kwa Diamond baba yake mzazi pamoja na kauli aliyoitoa baba huyo kwa mwanae diamond amefunguka upande wake pia. kwa sauti ya diamond mwenyewe akizungumza bonyeza hapa chini


Na hiki ndicho alichokizungumza kuhusu kauli ya TID pale alipomuita MPUMBAVU kwa kile kinachosemekana ANATUMIA jina la MNYAMA.



HAWA NDIO WASANII WALIOSOMA NA KWENDA SHULE PAMOJA


Ommy dimpoz mzee wa nai nai na baadae amesoma na super producer Mensen Selkta akiwa amemtangulia kidato kimoko pale Mbezi High school
Mesen Selekta yeye ni producer kutoka de fetality records lakini pia ni msanii ambae keshatoa pini kama kushoto kulia, na nyamnyamu.
Jaffarai amesoma na Jay moe kuanzia darasa la pili mpka la saba katika shule ya msingi Makumbusho iliyoka kijitonyama Dar-es-salaam

Juma Mchopanga a.k.a Jay moe
Mangwea mzee wa freestyle amesoma shule moja na Mez B, Noorah na Daki Master katika secondary ya Mazengo iliyoka Dodoma 
Mez B
Daki master
Noorah
Bob jr ambae pini lake la Nichumu limekamata nafasi ya kwanza ndani ya Top20 za Clouds wiki hii, amesoma na producer Nah Real ambae ameshatengenez pini kama Pea ya Nikki wa pili na zinginezo katika shule ya msingi Olympio.
Mzee wa Ndehe mtini Feruz amesoma na jamaa wa Born Cruz waliowahi kutoa ngoma iliyofanya vizuri iayoitwa kaka poa(wanamuita kaka poa huyu jamaa, wanamuita mtoto wa watu huyu jamaa) katika shule ya sekondari ya Makongo
Ben paul amesoma na Baghdadi Azania Secondary, lakini Ben Paul akiwa A level na Baghdadi akiwa A level
Baghdadi
Msanii Suma Lee amesoma na Producer Duke kutoka M lab katiska shule ya sekondari Sahare iliyoko Tanga huku Suma akiwa mbele ya Duke ki madarasa
Mh Temba kutoka kiumeni amesoma shule na Solo Thang, Rich one, Chidi Benz, Soggy Doggy, marehem Kanumba na Dazz baba katika shule ya sekondary ya Jitegemee iliyoko Temeke, Dar es salaam
Sollo Thang
Chidi benz
Marehem Kanumba

Thursday

IMEBAKI STORY--"HardMard"

NDOA YA HEMEDI YAKWAMA KISA ELIMU NDOGO


NDOTO kufunga pingu za maisha siku za karibuni alizokuwanazo nyota kutoka 'Bongo move' Hemed Suleiman 'PHD', zimeota mbawa kufuatia wazazi wa mlimbwende aliyetaka kumuoa kuweka ngumu.

katika mahojino mawili matatu Hemed amesema kuwa tayari alikuwa ameanza taratibu za kushughulikia ndoa yake na mrembo huyo iliyopangwa kufungwa kimya kimya kwa kuogopa watu wenye nia mbaya lakini amejikuta akilazimika kustisha harakati hizo kufuatia wazazi wa binti huyo wakaweka ngumu kwa madai kuwa wanataka mtoto wao amalize kwanza masomo yake na kupata 'mastaz' kwa kuwa elimu ya Degree aliyonayo hivi sasa wanahisi bado haijamtosha.

"unajua mchumba wangu hivi sasa ana elimu ya degree hivyo wazazi wamesema hawezi kuruhusujambo hilo kwanza mpaka apate 'mastaz' halafu ndiyo mambo mengine yatafuata, imeniuma sana kwa kuwa wenyewe tulishakubaliana na mwenzangu alikuwa tayari kwa hilo" alisema Hemed.

katika hatua nyingine Hemed amesema kuwa yuko katika hatua za mwisho kutoa muvi yake mpya aliyoibatiza jina la Mererani ndani yake akiwa amemshirikisha swahiba wake wa kitambo Yusuf Mlela sambamba na wakali wengine kibao wanaofanya kweli na Bongo move

DRAKE ATUMIA DOLA MILIONI 7.7 KUNUNUA NYUMBA LOS ANGELES.








Ataweza kumualika rafiki yake Serena William agonge Tennis kidizaini kwenye nyumba yake huku wakila bata

SHUGHULI YA KUTAFUTA MAITI ZANZIBAR


Meli ya Mv SKAGIT ikimalizikia kuzama jana katika eneo la Chumbe Zanzibar


Shughuli ya kutafuta maiti kwenye ajali ya meli iliyozama nchini Zanzibar ilianza mapema jana huku watu takribani miamoja wakiwa bado hawajapatikana baada meli iliyokuwa inaelekea kisiwani Zanziabr kuzama eneo la Chumbe.

Meli hiyo ilitoka Dar Es Salam  kuelekea kisiwani Zanzibar ikiwa imebeba watu miambili tisini.

Hadi kufikia sasa maiti 39 wamepatikana huku watu zaidi ya 150 wakiokolewa.

Msemaji wa polisi nchini Zanzibar aliambia shirika la habari la AFP kuwa kwa sasa kuna hofu ya kutopatikana manusura wowote waliokuwa katika meli hiyo ya MV Skagit

"shughuli ya kuwatafuta manusura na maiti inaendelea lakini kwa sasa ni vigumu kwa kweli kupata manusura." alinukuliwa akisema msemamji huyo wa polisi.

Tuesday

This was a July 4th show back in 2010 were Wakazi shared the stage
with Erica Lulakwa, Mercy Myra (Kenya), Roy Kapale (Uganda) and MukamaMorandi in Minneapolis, MN. Stay Tuned for more of Wakazi performancesVideos, as we are awaiting the Release of his EP, ABACUS.

DULLAH WA PLANET BONGO AFIWA NA MTOTO WAKE WA KIUME.

Abdallah Hamis Ambua wengi tunamjua kwa jina la Mjukuu wa Ambua Mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo kutoka East Africa Radio & TV leo majira ya saa 9 alasiri amempoteza mwanae wa kwanza wa kiume kuzaliwa. Mtoto huyo ambaye alikuwa na siku moja toka kuzaliwa hiyo jana mchana. 
Na haya ndio niliyoyakuta kwenye facebook ya Dullah

Hii ni status ambayo aliiandika jana mchana baada ya kupata mtoto na alikuwa na furaha sana na furaha hiyo nikampigia simu na kumpa hongera na kuanza kumuita baba na kumpa maneno mengi sana akiwa kama kijana mwenzangu ambaye yupo kwenye Ndoa

HII NDIO SHOW ILIYOFANYWA MJINI KIGOMA Leka Dutigite‬ @ Lake Tanganyika Stadium,


 Mh Zitto Zuber Kabwe akiongea na wananchi wa Kigoma

Lake Tanganyika Stadium ukiwa umetapika kwa wingi wa watu

  na Joshua Nassary

 Wabunge wakitgita

DIVA LOVENESS LOVE "ATAKAENIOA MAHARI SI CHINI YA MILIONI 500"



Mwana dadiva anaeendisha kipindi cha ala za roho ndani ya the people's station Diva loveness love hivi karibuni amefunguka alipokuwa akifanya kipindi cha xxl na mtu mzima Adam Mchomvu kuwa kwa yeyote atakae jitokeza kumuoa basi lazima awe na si chini ya shilingi millioni 500..Hii ni sooo baaaaaab!!!! JIPANGE

Kanye West Has A Special Cell Just For Kim?

kim kardashian kanye west mason disick

Whaaaat??
He might not have a problem tweeting up a storm, but according to close sources, Kanye West "hates being tied down to technology."
Specifically? A cell phone.
We're hearing that Kanye never liked using a cell phone before Kim Kardashian came around. And since they started dating, Kim's apparently forced him to get one.
One insider says:
"It frustrated Kim. She had to call him through a bodyguard. [So] he only uses it for Kim!"
Inneresting… though we're having a hard time believing Kim was the one introducing Kanye to the future…
C'mon… it's Yeezy! Ring Ring! Hello!
[Image via WENN.]

 

Thursday

P SQUIRE WAMPOTEZA MAMA YAO


Wasanii wakubwa nchini Nigeria na duniani kote, P-Square wamempoteza mama yao mzazi Mrs Okoye usiku wa kuamkia leo nchini India alipokuwa amepelekwa kwa matibabu baada ya kuhamishwa kutoka katika moja ya hospitali kubwa nchini Nigeria, St Nicholas iliyopo Yaba, Lagos.
inasemekana mama wa wasanii hao, alikua ni moja kati ya nguzo yao kubwa kimuziki kwa kuwapa ushauri na upendo usio na gharama yoyote.
arrangement zinafanyika ili kuurudisha mwili wa marehemu nchini Nigeria.

HEMED, MLELA: Hakuna kusubiri tena

NEW HIT: KigomAllStars - Leka Dutigite.



Kigoma All Stars MWASITI, BANANA ZORO, CHEGE, DIAMOND, ABDU KIBA, OMMY DIMPOZ, RECHO, LINEX, BABA LEVO, MAKOMANDO NA PETER MSECHU. 



Dhumuni na nia ya kutengeneza wimbo huu ni kuweka umoja wa watu wa kigoma na tanzania kwa ujumla. Pia watafanya show ndani ya kigoma wiki ijayo kwa ajili ya kusaidia wanafunzi na yatima ndani ya kigoma.

SOLO THANG aja na "MISS TANZANIA"


"JOGOO KICHAA"Aendeleza swaga la JAMBO SQUAD





                                        

Tuesday

Naibu Spika wa Bunge wa zamani afariki dunia

On Streets Today

Naibu Spika wa Bunge wa zamani, Mathias Michael Kihaule, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.

Kwa mujibu wa taarifa Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, jijini Dar es Salaam iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, alifariki Jumapili ya Mei 3, mwaka huu.

Kihaule ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Ludewa, mkoani Iringa, alizaliwa Julai 19, 1933 na amefariki akiwa na umri wa miaka 79.

Licha ya kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 15, kuanzia mwaka 1980-1995, Kihaule alilitumikia taifa katika wadhifa wa Naibu Spika wa Bunge.

Alikuwa na wadhifa huo katika kipindi chake cha tatu cha ubunge, kuanzia mwaka 1990 mpaka mwaka 1995.

Baada ya kipindi chake cha ubunge, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, kuanzia mwaka 1995 hadi 2004.

Katika utumishi wake wa umma, Kihaule amewahi pia kushika nyadhifa kadhaa kitaaluma, ikiwamo Mkufunzi wa Vyuo mbalimbali vya Ualimu nchini.

Hadi alipofariki, alikuwa akijihusisha na shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji, na atakumbukwa na wananchi wa Ludewa kwa jinsi alivyokuwa akishirikiana nao katika  maendeleo ya jimbo na wilaya yake kwa kipindi chote alichokuwa bungeni na mara baada ya kumaliza muda wake wa ubunge.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa mtoto wake, Dk Anold Kihaule, Ilala Maghorofani, ambako ibada ya kuaga mwili itafanyika leo Msimbazi Centre kuanzia saa 6 mchana, kabla ya kusafirishwa kesho kwa ndege kwenda Ludewa kwa mazishi.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin.
CHANZO: NIPASHE

Siri nzito yafichuka Chadema

On Streets Today

                   
                        Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
 
Maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imebainika kuwa ni sehemu ya mikakati yake inayolenga kuibua chuki za wananchi na kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Vyanzo vya habari ndani vya Chadema ambavyo havikutaka kutajwa majina yao, vimelieleza NIPASHE Jumapili kuwa, chama hicho kilifanya tathmini na kubaini kasoro zilizochangia kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Miongoni mwa kasoro hizo, ni ari ndogo iliyojitokeza kwa wananchi kulinda kura za wagombea urais na ubunge kupitia Chadema.
“Ili wananchi wawe tayari kuona umuhimu wa kulinda kura za chama cha siasa, inabidi wawachukie watawala, sasa tunachokifanya ni kueleza upungufu wa chama tawala ili wananchi waamke, waichukie CCM,” kilieleza chanzo hicho.
Hata hivyo, akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mahakama jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, pamoja na mambo mengine alisema chama hicho kitaendelea kuwachochea wananchi kuiasi CCM na kukiunga mkono chama chake.
Mbowe alisema, “wanasema Mbowe ni mchochezi, wanasema Chadema inapandikiza chuki, mimi na chama changu tutaendelea kuuhamasisha umma kuondokana na woga, wawachukie watawala walioshindwa kuwaletea maendeleo.”
Chadema imekuwa na utaratibu wa kuandaa maandamano na mikutano ya hadhara kupitia kile kinachojulikana kama operesheni maalum, mathalani kwa sasa ikijulikana kama Operesheni Okoa Kusini.
KUCHUKUA MFUMO WA CCM
Kwa upande mwingine, mkakati uliobuniwa na kuzinduliwa na Chadema, ukijulikana kama Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) umetajwa kama wenye lengo la kukisimika chama hicho hadi kwenye ngazi ya ubalozi, kama ilivyo kwa CCM.
Kupitia M4C Chadema inajikita kwa ‘kuvuna’ wanachama na kusimika uongozi katika ngazi tofauti kuanzia mabalozi, matawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hatimaye taifa.
Tayari Chadema kwa kutambua umuhimu wa kukiweka chama katika ngazi ya msingi (ubalozi), kimetumia ibara ya 7.1.1 ya Katiba yake kimeweka tarehe ya kufanyika uchaguzi nchi nzima.
Mbali na ngazi ya ubalozi, Chadema imetumia ibara ya 7.1.3 kutangaza uchaguzi wa chama hicho ngazi ya tawi, ambapo awali kilionekana kutokuwepo katika maeneo mengi ya nchi.
“Tunapoingia ndani ya jamii kufikia ngazi za msingi, tawi na kata, tutajihakikishia kuichukua nchi kwa urahisi zaidi,” kilieleza chanzo hicho.
Chadema imetoa maelezo ya taratibu za uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama hicho kwa ngazi za msingi na matawi, kikitumia ibara ya 11-1 ya chama hicho na kuzisambaza nchi nzima.
Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema, Msafiri Mtemelwa, alithibitisha kuchapishwa kwa maelezo hayo na kwamba yatafanikisha chaguzi hizo kufanyika kwa mujibu wa Katiba.
Maelezo hayo yanataja Septemba Mosi hadi Oktoba 5, mwaka huu kuwa siku za uchaguzi ngazi za msingi wakati ule wa matawi utafanyika kati ya Desemba 5 hadi Januari 8, mwaka ujao.
Chaguzi nyingine na ngazi zake kwenye mabano zitafanyika Februari 8 hadi Machi 14, mwaka ujao (kata), Aprili 14 hadi Mei 23, mwaka ujao (jimbo), Juni 23 hadi Julai Mosi, 2013 (wilaya) na Agosti 2 hadi Septemba 11 mwakani (mkoa).
Chaguzi zote hizo zitafanyika zikihusisha pia mabaraza tofauti ya Chadema, lile la vijana (Bavicha), wanawake (Bawacha) na Wazee.
Chanzo kimeeleza kuwa kupatikana kwa uongozi katika ngazi hizo kutaiwezesha Chadema kuwa na mtandao utakaohusika katika kulinda nafasi za wagombea uwenyekiti wa mitaa, vitongoji na vijiji, udiwani, ubunge na urais.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mwembe Mmoja (CCM) mkoani Mtwara , Abdallah Suleiman Mnyalu, alisema kazi za kisiasa hususani kukutana na kuzungumza na wananchi, zitaiathiri CCM katika chaguzi zijazo.
Alipotakiwa na NIPASHE Jumapili atoe maoni yake kuhusu athari za Chadema katika ngazi za msingi kwenye jamii, Mnyalu alisema chama hicho kinafanya kazi zilizopaswa kufanywa na CCM, lakini chama hicho tawala kimelala.
“Wenzetu hawa wanapita na kukutana na wananchi, lakini sisi wenye dola hatufanyi hivyo mpaka ufike Uchaguzi Mkuu,” alisema.
Mnyalu alisema pia kuwa vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na viongozi wa serikali katika ngazi za msingi vimechochea chuki ya wananchi kwa chama tawala, hivyo kutoa mwanya kwa wapinzani hususani Chadema kuungwa mkono.
MATUMIZI YA MTANDAO WA MAWASILIANO
Imebainika kuwa Chadema imejizatiti kutumia njia mbalimbali kuwafikia wapiga kura, wakiwemo wasiojitokeza na kushiriki shughuli za kisiasa hadharani.
Kupitia mkakati huo, imeelezwa kuwa chama hicho kitatumia njia ya mitandao ya kijamii iliyopo kwenye mawasiliano ya kisasa, kupenyeza kampeni na hoja zake.
MKAKATI WA KUJIENEZA
Kikiwa katika Operesheni Okoa Kusini inayoendelea kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara, Chadema kinawatumia viongozi na makada wake kufika maeneo ya vitongoji, vijiji na kata ambapo wanazungumza na wananchi, kufungua matawi na kusimika uongozi wa muda.
Jana, Chadema kilichoanza ziara zake mkoani Mtwara Mei 27, mwaka huu, kimeingia mkoani Lindi ambapo kitafanya mikutano ya hadhara na kufungua matawi yake hadi Juni 9, mwaka huu kitakapofanya mkutano wa hadhara mjini Lindi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Search This Blog