Tuesday
TAARIFA KUHUSU UKIMWI USIOSIKIA DAWA AFRIKA MASHARIKI NDIO HII.
Makao Makuu ya WHO Geneva.
Inawezekana stori nyingine huwa unazichukulia poa, lakini hii usiichukulie poa hata kidogo.
Ninachotaka kukwambia ni kwamba aina ya ugonjwa wa ukimwi ambao hausikii dawa umekua ukiongozeka kwenye hili bara la Afrika katika muda wa muongo mmoja uliopita.
Ninachotaka kukwambia ni kwamba aina ya ugonjwa wa ukimwi ambao hausikii dawa umekua ukiongozeka kwenye hili bara la Afrika katika muda wa muongo mmoja uliopita.
BBC wamesema, kuna ripoti ilimeandikwa na wataalam kwenye jarida la kisayansi la Lancet.
Wataalamu hao wamesema hali
hiyo ya ugonjwa kutosikia dawa huenda ikatokea ikiwa wagonjwa hawata
zingatia na kutumia dawa walizopewa na pia ufuatiliaji mbaya.
Hali hiyo inazusha hofu zaidi
katika bara la Afrika ambako hakuna njia mbadala ya kuwatibu wanaouguwa
maradhi ya Ukimwi ambapo watatifi kutoka shirika la Afya duniani-WHO na
chuo kikuu London wamegundua kwamba aina ya ukimiwi ambao hausikii dawa
unapatikana zaidi kwenye nchi za Afrika Mashariki.
Yani wanasema asilimia 26% ya
waathirika wako katika hali hiyo ikilinganishwa na asilimia 14 katika
nchi zilizo kusini mwa Afrika, Lakini kwenye nchi za Amerika, Afrika Magharibi na kati hakuna kitu kama hicho.
Chanzo kikubwa cha hayo yote ni
kwa sababu wagonjwa hawatumii dawa kama inavyotakiwa ambapo hii stori
imetoka siku tano tu baada ya kumsikia waziri mkuu Mizengo Pinda akisema
Tanzania imekua miongoni mwa nchi 36 duniani zilizofanikiwa kupunguza
maambukizi mapya ya UKIMWI kwa asilimia 25.
YOTE ALIYOSEMA DULLY SYKES KUHUSU CHUKI ZA WASANII WAKONGWE KWA WASANII WAPYA WENYE MAFANIKIO.
.
Inawezekana ukawa umesikia
sikia stori za baadhi ya wasanii wakubwa wa Tanzania kutopenda maendeleo
au mafaniko ya wasanii wapya wanaofanya vizuri this time.
Dully Sykes amekua msanii wa kwanza kujitokeza wakati huu na kukemea wasanii wakubwa wenye tabia hizo.
Amesema “Hilo lipo wazi, msanii
kama mimi nasikia raha sana vijana kama Diamond, Tunda Man, Mr Blue,
Ally Kiba na wengine wakifanya vizuri, kwa hiyo msanii mkubwa kama
utakua umeshindwa kufanikisha kile ulichotakiwa kukifanya alafu kijana
mdogo akafanya basi mpigie makofi, kama unaona huwezi kufika pale
unapotaka basi waachie vijana wafike, tusiwaingilie”
Kuhusu uwepo wa wasanii wakubwa
wenye wivu kwa wadogo wenye mafanikio, Dully kasema “Wivu utakuepo
unajua huwezi kuona kijana kaanza juzi tu alafu leo anafanya kitu kizuri
ukafurahia lakini sijui mimi nina moyo gani tofauti na wenzangu,
nafurahia sana vijana wakifanya vizuri kama Diamond, Linah, Amini,
Barnaba na wengine wanaofanya vizuri”
Kwenye line nyingine Dully
amesisitiza kwa kusema “sioni sababu ya mimi kumchukia mtu, sisi wasanii
wakongwe wazee ambao tupo kwenye game siku nyingi, tufurahie kazi ya
vijana wanayoifanya tumfurahie Diamond, Barnaba, Amini, Mr Blue na
wengine wote, tuwafurahie wale…….. na sio kwamba nimemsema mtu wala
kumlenga mtu”
HAYA NDIO MANENO 240 ALIYOYASEMA DIAMOND PLATNUMS KUMALIZA MJADALA NA BABA YAKE.
Baada ya stori kuandikwa kwenye
magazeti kwamba Staa Diamond Platnums anadaiwa kumtelekeza baba yake na
hamjali wala hataki kusikia stori zake, hii ndio kauli ya Diamond
kuhusu hiyo ishu.
Amesema “kiukweli ni vitu
ambavyo mimi vimenishangaza sana kwa sababu sijui chochote nakuja kukuta
tu kwenye magazeti, na nisingependa nisikie swala la mzazi wangu kusema
mimi ni mtoto wake sijui nini na nini kwamba mimi nafanya starehe
sihusiki na yeye sio kauli nzuri kiukweli, ina maana ananijua kwamba
mimi ni mwanae baada ya kuwa DIAMOND”
Kwenye line nyingine Diamond
amesema “siku zote kama alijua mimi ni mtoto wake basi angenisomesha na
kunipa elimu nzuri lakini siku zote nilihangaika na Mama yangu mzazi
akanikuza na kunisomesha kwa shida na tabu zote mpaka leo nimekua hivi,
nisingependa kumsikia mtu yeyote anaongea kwamba mimi ni mtoto wake au
yeye ni nani kwa sababu siku zote hawakuonekana, wasitake kuonekana
kipindi cha Maslahi mtu ndio anajifanya anahusika sana na mimi kama
mtoto wake”
“Haya mambo nilianza kuyasema
toka natoa single ya binaadam sikujua hata kama leo ningekuja kuwa na
Prado, makazi au kuwa na haya mafanikio mengine, baba yangu ataendelea
kuwa baba yangu tu ila siwezi kumpa kipaumbele kama ninachompa mama
yangu kwa sababu kama angetaka hilo angenijali toka mapema” – DIAMOND.
Kwa kumalizia, Diamond ambae
mpaka sasa ametumia zaidi ya milioni 69 kujenga Nyumba yake Tegeta Dar
es salaam amesema “mimi nilikua napenda kusoma na nilikua nafanya vizuri
kwenye masomo yangu lakini sikua na uwezo wa kifedha kuendelea kusoma,
mzazi wangu alikua na pesa ina maana angenijua mimi angenisomesha leo
ningekuja kuwa hata mbunge au hata waziri kwa sababu mi najua nina upeo
mkubwa sana wa kielimu na vitu vingine, sasa nimesota na muziki alafu
leo ndio wanajitokeza, SITAKI WANIACHE NA MAMA YANGU MZAZI”
MOVIE MPYA YA BATMAN YAZUA KIZAA ZAA NCHINI MAREKANI
Filamu mpya ya Batman inayoitwa The Dark Knight Rises imeanza kuonyeshwa jana.Filamu hiyo ambayo imechezwa na Christian Bale imeanza kuonyeshwa nchini Marekani jana katika kumbi mbali mbali za sinema.Watu wengi waliojitekeza katika Theater ya 16 century Colorado wamekumbwa na maafa baada ya mtu asiefahamika kuingia na kupiga risasi hovyo.Watu zaidi ya 12 wamepoteza maisha akiwemo mtoto wa miaka 12,70 wamejeruhiwa pia yumo mtoto wa miezi mitatu.
Mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina
la James Holmes mwenye miaka 24.Aliingia ukumbini humo akiwa kavalia
kama mmoja wa wahusika ambae amecheza kama adui katika filamu hiyo Tom
Hardy aliyetumia jina la Bane.Anaonekana pichani.Alipoingia akatupa bomu
la moshi na kisha kuanza kurusha risasi hovyo.
Wanafamilia mbali mbali wakifarijiana
Baba ambae mtoto wake wa miezi mitatu alipigwa risasi ya mgongoni akiwa hospital katika hali ya huzuni na kuchanganyikiwa.
Miongoni wa waliofariki yupo
dada mtangazaji wa tv Jessica Ghawi.Muda wote akiwa katika jumba la
sinema alikuwa akitweet namna anavyofurahia movie hiyo mpaka mauti
yalipomkuta.
Tukio hilo limetokea jana usiku
katika mji Colorado eneo linaitwa Aurora.Rais wa Marekani Barack Obama
ametuma salamu zake za rambi rambi kwa wafiwa na kuwaomba wanachi wake
kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu.Pia akawaomba kuwaombea wakazi
wa eneo hilo waweze kupita katika wakati huo ambao umewaacha katika
mshituko.
Sunday
Washindi wa Tuzo za Zuku Kutangazwa ZIFF
(July 17, 2012) Washindi wa Tuzo tatus za Zuku zilitangazwa wakati wa kufungwa rasmi wa tamasha la ZIFF. Tuzo za Zuku ni jamii mpya za tuzo ambazo zimefanikishwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la ZIFF. Tuzo hizo zili wazawadia filamu zenye ubunif wa kuelezea hadithi za kiafrika, zilizotengenezwa Afrika, na watengenezaji na wasanii kutoka bara la afrika.
Akizungumza wakati wa kutoa tuzo, Wangeci Murage Zuku alisema, "Tunafurahia sana kuanzisha tuzo mpya katika tamasha la ZIFF na lengo letu ni kukuza tuzo hizi hadi ziwe mojawapo wa tuzo za kifahari hapa Afrika”.
Mwaka huu, tuzo la Zuku Best African Film Award lilipewa filamu ya ‘Inside Story’ kutoka Rwanda iliyotayarishwa na Rolie Nikiwe. Tuzo la Zuku Best Actor Tuzo lilishindwa na mwigizaji Kevin Ndege Mambo ambaye alifanya kazi kama katika filamu ya ‘Inside Story’. Tuzo la Zuku Best Actresslilishindwa na waigizaji wanawake watatu yaani Thuli Khulamelo, Nomfundo Dunazana na Reona Ngiba ambaye waliigiza katika filamu ya ‘Uhlanga the mark’
Tuzo za Ousmene Sembene Award and Verona Award na Tuzo la ZIFF Golden Dhow Award zilishindwa na mfilmau ya ‘Uhlanga the mark’. Tuzo la ‘ZIFF Best Short Film’ lilishindwa na Filamu‘Mocassin’ iliyotayarishwa na Denis M. Kimathi. Tuzo la ZIFF Best Documentary Award, lilishindwa na filamu ya “Mama Africa” iliyotayarishwa na Mika Kaurismaki. Tuzo la ZIFF Best Animation Award lilipewa “Ostora” iliyotayarishwa na Hani Kichi
Kwa upande wa filamu za Tanzania, ‘Zamora’ iliyotayarishwa na Shams Bhanji iliweza kutwa tuzo mbili za filamu bora afrika mashariki na filamu. Filamu ya “Chungu” iliyotayarishwa na Kiela Billailiwea kutwaa tuzo ya filmau bora ya ZIFF.
Zuku ambayo ni kampuni ya TV ya kulipia ambayo inaendelea kukua kwa kasi inapatikana Tanzania, Uganda na Kenya, ina nia ya kudhamini ZiFF kwa kipindi cha miaka 10 kwa thamani ya jumla ya dola milioni moja. Udhamini huo unatarajiwa kutoa utulivu na msaada ambayo kwa upande utachangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha sekta ya filamu, si tu nchini Tanzania lakini maeneo mengine ya Afrika.
Kingamuzi cha Zuku kinatoa wigo mpana wa uchaguzi wa burudani ka vile habari za michezo, sinema, makala na muziki. Hizi ni pamoja na chaneli tatu za BBC World News, MTV Base, Setanta Sports, Fox Entertainment na E!. Zuku pia inatoa chanelli zingine kama Zuku AFrika, Zuku Life, Zuku Sports na Zuku Movies. Huduma hii patikana kupitia satellite mahali popote Tanzania
MWISHO
Ngoma Africa band inawatakia Ushindi Wanamichezo wa Tanzania olympic 2012
Ngoma Africa band
inawaombea USHINDI wanamichezo wa Tanzania Olympic London 2012
FFU watoa wito kwa watanzania kuwapa shavu wanamichezo wetu !Olympic
Watanzana wameombwa kujitokeza kwa wingi katika kuwashingilia wanamichezo watanzania wanaoshiriki
katika michezo ya Olympic huko London, wito huo umetolewa na bendi maarufu ya Ngoma Africa aka FFU,
yenye makao yake Ujerumani.
Bendi ya Ngoma Africa inawaombea mafanikio na ushindi wanamichezo wa Tanzania,
Tuwaomba watanzana na marafiki wa Tanzania pamoja taha sisi mbali mbali zilizopo Uingereza na ughaibuni
kujitokeza kwa wingi na kuzipeperusha bendera za Tanzania kwa kuwashingilia wanamichezo wetu,kwa shangwe,
shangwe na mayoe ! Tanzania ! Tanzania! Tanzania! oyeeeeeeeeeee!
Mungu wabariki wanamichezo wetu! www.ngoma-africa.com
BODI YA MASHINDANO YAFUTA NA HAITAMBUI MISS UTALII KANDA YA ZIWA 2012
Bodi ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO),imefuta na
kutokulitambua shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012 lililo
fanyika New Mwanza Hotel ,wakati taifa likiwa katika maombolezo ya
msiba mkubwa wa kitaifa wa watu waliopoteza maisha katika ajali ya
meli iliyo tokea Zanzibar.
kutokulitambua shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012 lililo
fanyika New Mwanza Hotel ,wakati taifa likiwa katika maombolezo ya
msiba mkubwa wa kitaifa wa watu waliopoteza maisha katika ajali ya
meli iliyo tokea Zanzibar.
Bodi imechukua hatua ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ambalo
limefanyika bila ya kuzingatia misingi ya kibinadamu na hata uzalendo
kwa Taifa. Waandaaji wa shindano hilo Fania Hassan wa Fania Beauty
Salon,pamoja na kutambua kuwa taifa lipo katika maombolezo ya siku
tatu kwa tangazo na tamko la serikali, bado hakuzingatia maelekezo ya
waandaaji wa Taifa ambao walisitisha mashindano ya Miss Utalii
Tanzania katika ngazi zote,likiwemo lile la Miss Utalii Kinondoni 2012
ambalo lilikuwa lifanyike tarehe 20-7-2012 katika ukumbi wa Traveltine
Dar es Salaam ambalo sasa litafanyika 31-7-2012 katika ukumbi wa Club
Maisha Oyterbay na lile la Miss Utalii Ilala 2012 ambalo lilikuwa
lifanyike 21 -7-2012 katika ukumbi wa Eriado View pont Pugu Dar es
Salaam ambalo sasa lifanyika siku ya Iddy Pili katika ukumbi wa Eriado
point View Pugu.
limefanyika bila ya kuzingatia misingi ya kibinadamu na hata uzalendo
kwa Taifa. Waandaaji wa shindano hilo Fania Hassan wa Fania Beauty
Salon,pamoja na kutambua kuwa taifa lipo katika maombolezo ya siku
tatu kwa tangazo na tamko la serikali, bado hakuzingatia maelekezo ya
waandaaji wa Taifa ambao walisitisha mashindano ya Miss Utalii
Tanzania katika ngazi zote,likiwemo lile la Miss Utalii Kinondoni 2012
ambalo lilikuwa lifanyike tarehe 20-7-2012 katika ukumbi wa Traveltine
Dar es Salaam ambalo sasa litafanyika 31-7-2012 katika ukumbi wa Club
Maisha Oyterbay na lile la Miss Utalii Ilala 2012 ambalo lilikuwa
lifanyike 21 -7-2012 katika ukumbi wa Eriado View pont Pugu Dar es
Salaam ambalo sasa lifanyika siku ya Iddy Pili katika ukumbi wa Eriado
point View Pugu.
Bodi ya mashindano katiaka kikao chake cha dharula kilichofanyika leo
asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyanzo vyetu vya
uhakika,juu ya kufanyika kimyakimya kwa shindano hilo imeamua kuchukua
hatua hiyo kali ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ili iwe
fundisho kwa waandaaji wengine wasiozingatia maagizo kwa mujibu wa
kanuni na taratibu za mashindano haya.
Bodi imesikitishwa sana na tukio hilo kisilo la kizalendo, na
inawaomba radhi watanzania wote,ndugu na jamaa wote waliopoteza ndugu
zao katika ajali hiyo,serikali, mamlaka zote za mkoa wa Mwanza,
mamlaka za sanaa,wadhamini na wadau mbalimbali wa mashindano ya urembo
utalii na utamaduni nchini na nje ya nchi.
asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyanzo vyetu vya
uhakika,juu ya kufanyika kimyakimya kwa shindano hilo imeamua kuchukua
hatua hiyo kali ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ili iwe
fundisho kwa waandaaji wengine wasiozingatia maagizo kwa mujibu wa
kanuni na taratibu za mashindano haya.
Bodi imesikitishwa sana na tukio hilo kisilo la kizalendo, na
inawaomba radhi watanzania wote,ndugu na jamaa wote waliopoteza ndugu
zao katika ajali hiyo,serikali, mamlaka zote za mkoa wa Mwanza,
mamlaka za sanaa,wadhamini na wadau mbalimbali wa mashindano ya urembo
utalii na utamaduni nchini na nje ya nchi.
Washiriki wote watalazimika kusubiri tarehe mpya ya kufanyika kwa
shindano hilo,baada ya mfungo wa ramadhani,ambapo pia watagharamiwa
gharama zote za ushiriki wao upya,kama kanuni na taratibu za
mashindano zinavyo bainisha kuwa washiriki wote wa mashindano ya Miss
Utalii tanzania wanagharamiwa gharama zote za
mavazi,usafiri,vinywaji,chakula na saluni.
Kamati ya nidhamu ya mashindano haya itakutana mwisho wa mwezi ili
kujadili hatua zaidi za kuchukua dhidi ya waandaaji hao wa Miss Utalii
kanda ya Ziwa 2012.
Haiwezekani hata kidogo wakati taifa lina omboleza halafu mtu anatumia
mashindano haya ambayo ni alama ya urithi wa Taifa na kielelezo cha
utamaduni wa mtanzania kukiuka utamaduni,mila na desturi za
Tanzania,tena wakati hata serikali imetangaza maombolezo na bendera
zinapepea nusu mlingoti.
Kwa mara nyingine tena tunaungana na watanzania wote kuwapa pole Ndugu
zetu wa Zanzibar walio Potelewa na ndugu jamaa pamoja na Marafiki,
Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape Nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Pia kwa wale majeruhi na ambao wapo kwa matibabu pia Tunawaombea
wapate kupona Haraka ili warejee katika kazi zao za kujenga taifa.
Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa – Utalii ni Maisha
,Utamaduni ni Uhai wa Taifa.
Asante,
Abubakari Omary Bakari
MKURUGENZI WA UTAWALA NA FEDHA - MISS TOURISM TANZANIA ORGANISATION (MTTO)
shindano hilo,baada ya mfungo wa ramadhani,ambapo pia watagharamiwa
gharama zote za ushiriki wao upya,kama kanuni na taratibu za
mashindano zinavyo bainisha kuwa washiriki wote wa mashindano ya Miss
Utalii tanzania wanagharamiwa gharama zote za
mavazi,usafiri,vinywaji,chakula na saluni.
Kamati ya nidhamu ya mashindano haya itakutana mwisho wa mwezi ili
kujadili hatua zaidi za kuchukua dhidi ya waandaaji hao wa Miss Utalii
kanda ya Ziwa 2012.
Haiwezekani hata kidogo wakati taifa lina omboleza halafu mtu anatumia
mashindano haya ambayo ni alama ya urithi wa Taifa na kielelezo cha
utamaduni wa mtanzania kukiuka utamaduni,mila na desturi za
Tanzania,tena wakati hata serikali imetangaza maombolezo na bendera
zinapepea nusu mlingoti.
Kwa mara nyingine tena tunaungana na watanzania wote kuwapa pole Ndugu
zetu wa Zanzibar walio Potelewa na ndugu jamaa pamoja na Marafiki,
Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape Nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Pia kwa wale majeruhi na ambao wapo kwa matibabu pia Tunawaombea
wapate kupona Haraka ili warejee katika kazi zao za kujenga taifa.
Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa – Utalii ni Maisha
,Utamaduni ni Uhai wa Taifa.
Asante,
Abubakari Omary Bakari
MKURUGENZI WA UTAWALA NA FEDHA - MISS TOURISM TANZANIA ORGANISATION (MTTO)
STREET NA MATUKIO
STAA wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu na kichwa kinachotingisha katika Bongo Fleva, Nasib Abdul Juma ‘Diamond’ wamenaswa wakiwa beneti mkoani Kigoma.
Chanzo kilichopo mkoani humo, kimepenyeza habari hiyo juzi, ambapo kilisema ukaribu wao uliamsha hisia kwamba huenda wawili hao wamerudiana.
“Wapo wote huku Kigoma, kwa Diamond ni sawa maana yupo na wasanii wenzake wa Kigoma All Stars, sasa Wema amekujaje? Kwanza siyo mwanamuziki, lakini pia siyo mtu wa Kigoma ni wa kutoka Tabora,” kilieleza chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hiyo, Ijumaa lilimvutia waya Diamond zaidi ya mara tatu lakini simu iliita bila kupokelewa.
Wema alipopigiwa simu alipatikana na kufafanua ishu nzima ilivyo. Huyu hapa msikie: “Ni kweli nipo huku Kigoma lakini sipo na Diamond. Nimekuja kwa mwaliko wa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini).
“Mimi na Diamond ni marafiki tu, hatuwezi kuwa wapenzi tena, kila mtu na maisha yake. Kifupi nina mtu wangu ambaye tunapendana na kuheshimiana sana.”
Alipotakiwa kumtaja mpenzi wake mpya alisema: “Kwa sasa siwezi kumtaja, lakini siku si nyingi nitamuweka hadharani watu wamjue.”
HATIMAE MTOTO WA KAMBO WA USHER RAYMOND AFARIKI DUNIA
Kyle Glover ambae ni mtoto wa mke wa zamani wa Mwimbaji Usher Raymond, amefariki dunia leo kutokana na kuumia kwenye ajali ya pikipiki za kwenye maji maarufu kama Jetski mwanzoni mwa mwezi huu huko Georgia Marekani.
Madaktari wametoa mashine zilizokua zinasaidia kumuweka hai mtoto huyo aliekua na umri wa miaka 11 baada ya kugundua kwamba majeraha aliyoyapata yasingeweza kutibika.
Kyle akiwa na rafiki yake wa kike mwenye umri wa miaka 15 walipata ajali july 8 2012 huko Georgia baada ya Inner tube waliyokuwemo iliyokua ikivutwa na boti kugongwa na Jetski wakiwa kwenye maji na hivyo kupata majeraha ya kichwa.
NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOFIKA KUMTEMBELEA KAJALA GEREZANI
Pichani ni washkaji zake Kajala walioenda kumtembelea mida hii pale gereza la Segerea na kuanzia kushoto ni Producer Lamar, Producer P.Funk Majani mbele yake ni Shilole msanii wa Bongo Fleva na anayefuatia ni B12 kutoka Clouds FM, VJ Penny, Sam Misago kutoka EATV na meneja wa Ommy Dimpozi anaitwa Muba.
HIKI NDICHO ALICHOKIZUNGUMZA DIAMOND KUHUSU KUTO0KUELEWANA NA BABA YAKE MZAZI NA KAULI ALIYOITOA TID JUU YAKE
Baada y amagazeti kuandika juu ya kutokuelewana kwa Diamond baba yake mzazi pamoja na kauli aliyoitoa baba huyo kwa mwanae diamond amefunguka upande wake pia. kwa sauti ya diamond mwenyewe akizungumza bonyeza hapa chini
Na hiki ndicho alichokizungumza kuhusu kauli ya TID pale alipomuita MPUMBAVU kwa kile kinachosemekana ANATUMIA jina la MNYAMA.
HAWA NDIO WASANII WALIOSOMA NA KWENDA SHULE PAMOJA
Ommy dimpoz mzee wa nai nai na baadae amesoma na super producer Mensen Selkta akiwa amemtangulia kidato kimoko pale Mbezi High school
Mesen Selekta yeye ni producer kutoka de fetality records lakini pia ni msanii ambae keshatoa pini kama kushoto kulia, na nyamnyamu.
Jaffarai amesoma na Jay moe kuanzia darasa la pili mpka la saba katika shule ya msingi Makumbusho iliyoka kijitonyama Dar-es-salaam
Juma Mchopanga a.k.a Jay moe
Mangwea mzee wa freestyle amesoma shule moja na Mez B, Noorah na Daki Master katika secondary ya Mazengo iliyoka Dodoma
Mez B
Daki master
Noorah
Bob jr ambae pini lake la Nichumu limekamata nafasi ya kwanza ndani ya Top20 za Clouds wiki hii, amesoma na producer Nah Real ambae ameshatengenez pini kama Pea ya Nikki wa pili na zinginezo katika shule ya msingi Olympio.
Mzee wa Ndehe mtini Feruz amesoma na jamaa wa Born Cruz waliowahi kutoa ngoma iliyofanya vizuri iayoitwa kaka poa(wanamuita kaka poa huyu jamaa, wanamuita mtoto wa watu huyu jamaa) katika shule ya sekondari ya Makongo
Ben paul amesoma na Baghdadi Azania Secondary, lakini Ben Paul akiwa A level na Baghdadi akiwa A level
Baghdadi
Msanii Suma Lee amesoma na Producer Duke kutoka M lab katiska shule ya sekondari Sahare iliyoko Tanga huku Suma akiwa mbele ya Duke ki madarasa
Mh Temba kutoka kiumeni amesoma shule na Solo Thang, Rich one, Chidi Benz, Soggy Doggy, marehem Kanumba na Dazz baba katika shule ya sekondary ya Jitegemee iliyoko Temeke, Dar es salaam
Sollo Thang
Chidi benz
Marehem Kanumba
Subscribe to:
Posts (Atom)
Search This Blog






















.jpg)








