Friday

KUHUSU JAMIE FOXX KUKATAA KUKUTANA NA BABA YAKE MZAZI.

On Streets Today
         

Jamie Foxx.

Stori kutoka the Box ni kwamba movie star ambae ni mwimbaji pia Jamie Foxx amekataa kabisa kuonana na baba yake mzazi ambae ni mgonjwa kwa sasa.

Sababu pekee inayofanya Jamie asitake kuonana wala kumsamehe baba yake ambae ana umri wa miaka 74 ni kutokana na mzazi huyo kumtelekeza akiwa mdogo.

Jamie alilelewa na bibi yake ambae alifariki mwaka 2004, toka mwaka huo Jamie hajawahi kuongea na baba yake mzazi.

Kwa sasa baba yake mzazi ni mgonjwa sana na amekua akihitaji kuonana na Jamie ili wayamaliza lakini staa huyu amekataa.

Mke wa sasa wa baba yake Jamie amekaririwa akisema “tumekua tukimpigia simu Jamie kwa miaka sasa lakini hapokei na wala hajawahi kujibu mamia ya msg tulizomuandikia, na sasa baba yake ni mgonjwa na anapumulia mashine… natamani Jamie apige simu”

Ni mastaa wengi wa dunia mpaka sasa ambao wamekua kwenye uhusiano mbaya na baba zao akiwemo Beyonce, Kelly Rowland nae alikua haongei na baba yake, movie star Angelina Jolie mpaka sasa bado hayuko kwenye uhusiano mzuri na baba mzazi.

UNAAMBIWA HILI NDIO GARI ANAMILIKI VIDEO QUEEN WA YOU GUY YA P UNIT KENYA

On Streets Today





Kwa mujibu wa mtandao wa Ghafla Kenya, yule mrembo alieng’aa kwenye video ya single mpya ya P Unit (You Guy) ambayo imefungiwa na kituo cha CITIZEN TV aitwae Vee Beiby anamiliki huu mkoko hapa, BMW Z3 Roadster.

Unaweza kumchek kwenye interview hapa chini na pia kwenye hiyo video ya P Unit chini yake.

                       


Video ya mwisho ni behind the scene ya wakati video ya ‘You guy’ ikitengenezwa.

TAARIFA KUHUSU DHAMANA YA MWIGIZAJI LULU AMBAYO ILIKUA ITOKE LEO.


On Streets Today

Elizabeth Michael. Jana kwenye allstreetsonline.com kulikua na stori kwamba uwezekano wa mwigizaji Lulu kuachiwa kwa dhamana january 25 2013 ulikuepo.


Ni kweli ilikua iwe hivyo lakini kwa taarifa zilizotolewa na vyombo husika ni kwamba dhamana hiyo imeshindikana kutolewa leo.


Sababu kubwa ni leo kuwa sikukuu hivyo shughuli imesogezwa mbele mpaka jumatatu january 28 2013.


Mwanzoni Lulu ambae anatuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia ilidaiwa alikua anatakiwa apate dhamana ambayo milioni 20 zilihitajika (kwa mujibu wa taarifa za ndani) ila ikashindika sababu jaji alipata udhuru.


Lulu amekua chini ya ulinzi toka kifo cha mwigizaji staa wa movie Tanzania Steven Kanumba April 2012.

ISOME TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA JAN 25 IKO HAPA

On Streets Today
WILAYA YA MOMBA – KUVUNJA CHUMBA CHA GUEST MCHANA NA KUIBA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani

MNAMO TAREHE 24.01.2013 MAJIRA YA SAA 10:30HRS HUKO KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO SERENGETI ILIYOPO TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. JOYCE D/O KEMTO,MIAKA 38,MFANYABIASHARA,MKISII MKAZI NA RAIA WA NCHINI KENYA ALIYEKUWA AMEPANGA KATIKA CHUMBA NO.06 ALIIBIWA PESA TSHS 150,000/= ZILIZOKUWA KWENYE MKOBA NDANI YA CHUMBA HICHO. WATUHUMIWA WAWILI 1.EMANUEL S/O CHARLES, MIAKA 40, MZANAKI, MKULIMA MKAZI WA MAGOMENI DSM NA 2. GODFREY S/O BENARD @ SIMFUKWE,MIAKA 42,MUHA,MKULIMA MKAZI WA MWANDIGA KIGOMA WAMEKAMATWA WAKIWA NA MKOBA WENYE PESA HIZO. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUPANGA CHUMBA JIRANI NA MHANGA NA KISHA KUFUNGUA MLANGO WA CHUMBA KWA KUTUMIA FUNGUO BANDIA WAKATI MHANGA AKIWA NJE. MHAMGA ALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA BAADA YA KUWAONA WATUHUMIWA WAKIWA NA MKOBA WAKE NA NDIPO WANANCHI WALIPOANZA KUWASHAMBULIA KWA KUWAPIGA MAWE NA FIMBO HATA HIVYO WALITOKEA ASKARI POLISI NA KUWAOKOA. MTUHUMIWA GODFREY S/O BENARD @ SIMFUKWE HALI YAKE NI MBAYA AMELAZWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA NA MWENZAKE ANAENDELEA KUSHIKILIWA POLISI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA PINDI WANAPOWAKAMATA WAHALIFU NA BADALA YAKE KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE. AIDHA ANATOA RAI KWA WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI KUIMARISHA ULINZI MUDA WOTE KATIKA BIASHARA ZAO. PIA ANAWAKUMBUSHA KUTOA TAARIFA HARAKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILISHA SHAKA AMBAO WANAFIKA KAMA WATEJA ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.

WILAYA YA KYELA – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MNAMO TAREHE 23.01.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IBANDA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. POLISI WALIWAKAMATA WATU WATANO RAIA WA NCHINI BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI AMBAO NI {1}.ALAKEZA S/O MOSE,MIAKA 32 {2}. BULALAHUBWA S/O KALODATI, MIAKA 25 {3}. ALAKAZYA S/O ALINI, MIAKA 6 {4}. NISHUNA D/O DORINA, MIAKA 6, NA {5}. MUNYEZE D/O JOZINA, MIAKA 9 . MBINU ILIYOTUMIKA NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO NA KUKUTWA KATIKA KANISA LA BABTISTI KIJIJINI HAPO WAKIOMBA HIFADHI. WATUHUMIWA WAMEKABIDHIWA IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KWA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU.

WILAYA YA MBOZI – KUSALIMISHWA KWA SILAHA MOJA AINA YA GOBOLE

MNAMO TAREHE 23.01.2013 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IYULA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. MTU/WATU WASIOFAHAMIKA WALISALIMISHA /TELEKEZA BUNDUKI MOJA AINA YA GOBOLE YENYE NAMBA – TOWKK 340. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUTELEKEZA SILAHA HIYO JIRANI NA KITUO KIDOGO CHA POLISI IYULA NA POLISI KUICHUKUA . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWAFICHUA KWA KUTOA TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAOMILIKI /TENGENEZA SILAHA BILA KIBALI ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANATAHADHARISHA WAMILIKI/WATENGENEZAJI HARAMU WA SILAHA HIZO KUZISALIMISHA HARAKA INGAWA MUDA WA “OFFER” UMEMALIZIKA KULIKO KUSUBIRI KUKAMATWA.

WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 24.01.2013 MAJIRA YA SAA 18:56HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NZIGWA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1.MAKENZA S/O IGEMBE, MIAKA 45, MSUKUMA, MKULIMA NA 2. MILEMBE D/O MALA,MIAKA 65,MSUKUMA MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA NZIGWA WAKIWA WANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA NUSU EKARI . WATUHUMIWA NI WAKULIMA NA WAUZAJI WA BHANGI. BHANGI YOTE IMETEKETEZWA KWA KUCHOMWA MOTO SHAMBANI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WAMILIKI NA MAHALI YALIPO MASHAMBA YA BHANGI KUZITOA KWA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA DHIDI YA WAHUSIKA ZICHUKULIWE.

Signed By,

[DIWANI ATHUMANI – ACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Thursday

PICHA NA TAARIFA ZA VURUGU ZINAZOENDELEA KIBITI RUFIJI SASA HIVI, WANANCHI WAMEVAMIA POLISI.. WANACHOMA

On Streets Today

Mwandishi Mrokim waFather Kidevu Bloganaripoti kwamba kundi la wananchi wenye hasira wamevamia kituo cha Polisi Kibiti Wilayani Rufiji na kuleta vurugu kubwa kutokana na raia mmoja kufa kwa kile kilichodaiwa kuwa kipigo cha Polisi.
Aliyefariki ni Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Muhimbili.

Habari za sasa ni kwamba wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari Polisi zilizopo jirani na kituo hicho licha ya juhudi za Polisi kuwatawanya kwa mabomu, pia wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti, hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya watu.

LULU KUACHIWA KWA DHAMANA.

On Streets Today



Taarifa za uhakika nilizozipata kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Lulu akatoka kwa dhamana kesho january 25 2013.

Uhakika wa Lulu kupata dhamana ulikua jana jumatano january 23 lakini ikawa imeshindikana kutokana na kuahirishwa kwa sababu jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua hakijatimia.

Chanzo cha kuaminika kilichoongea na millardayo.com kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.

Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba, endelea kuipitia millardayo.com kwa stori zaidi.

Saturday

MABESTE: HIZI NDIZO NGOMA ZANGU ZILIZOFANYA MPAKA MASHABIKI KUNIKUBALI KATIKA MUZIKI



PICHA YA WEMA SEPETU YAZUA GUMZO MITANDAO YA JAMII

Ikiwa ni mda mchache tu baada ya kupost picha zake zenye kuonyesha wazi sehem za tumbo na kifua kupitia Instagram, picha ya wema imeonekana kusambaa kwa haraka zaidi kupitia mtandao wa jamii "facebook" huku kila mmoja akitoa maoni yake kutoka na mtazamo wake. 
Obedy Bernard Hakika Ney wa mitego hakukosea, makahaba wenye vwango wako bongo move. Wema ni mfano tosha usio pngika kwa hilo. Halafu inakuwaje mwanatme mwenye akili zako umshobokee kahaba kama huyu? Yaani zkitoka tunzo za khb bora tz huyu malaya hatakuwa na mpinzani.

Timoth Kalavuze wema noma xnaa!!!

Hija Punch Boy Mbogo no one like you i love you wema sepetu waache waogee 2 kwamba wewr malaya kwangu wewe ni namba moja

Paul Shangal Hamna kioo cha jamii bali ktanda cha jamii


Shabbani Saidi daaaaaaaaa ujuwe dada zetu wana tabu sana naiyote kutaka kufosi kuwa maalufu kama watu wa mbele kumbe awajui kama wana jizalilisha kwani lazima uwe malufu na tama ina wapoza kk tuseme ukweli bwana

Mary Talalela usi judge na ku-coment bad about her mwache ahave funny nyie mnajua wake au magirlfnd zenu huwa wanafanya nini nyuma ya pazia ....? sibora wema .... i love u baby wema sana shoo what u have.

kupitia Instagram wema alipost picha hiyo ikiwa na maneno haya " gats to lose me a few more pounds"

PICHA:DIAMOND AKITANGAZA LIVE KIPINDI CHA COUNTDOWN NDANI YA CHOICE FM

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa msanii wa Bongo Fleva maarufu kama Diamond Platinum kwa kuwasha kipaza sauti na kuendesha show ya redio kwa masaa mawili live ndani ya choice Fm 102.5 Fm Hebu tune to Choice Fm today kuanzia hivi sasa 3pm-5pm.


BRANDTS AIONGOZA YANGA KATIKA MECHI YA 14 LEO

Brandts 

KOCHA Mholanzi, Ernie Brandts leo anatarajiwa kuiongoza Yanga katika mechi ya 14 tangu ajiunge nayo Septemba mwaka jana, akitokea APR ya Rwanda wakati itakapomenyana na Black Leopard ya Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Yanga SC iliyorejea wiki Jumapili kutoka Uturuki kwenye kambi ya wiki mbili mjini Antalya, imekuwa ikijifua katika Uwanja wa Mabatini, Kijitonyama tangu Jumatano kwa ujumla kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
Yanga leo itakutana na Black Leopard inayoshika nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini yenye timu 16, iliyowasili jana Dar es Salaam ikiwa na msafara wa watu 42 na kufikia katika hoteli ya White Sands, Mbezi Beach, Dar es Salaam. 
Wachezaji wote walifanya mazoezi jana, kasoro kipa wa tatu, Yussuf Abdul na mshambuliaji Hamisi Kiiza 'Diego' wanaosumbuliwa na Malaria. 
Katika mechi 13 ambazo Brandts ameiongoza Yanga hadi sasa tangu arithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, ameshinda saba, kafungwa nne na kutoka sare mbili. 
Kati ya hizo, mechi tisa ni za Ligi Kuu, ambazo amefungwa moja tu dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba, wakati nyingine dhidi ya watani wa jadi, Simba SC alitoa sare ya 1-1 na saba ameshinda dhidi ya Toto African 3-1, Ruvu Shooting 3-2, Polisi Moro 3-0, JKT Oljoro 1-0, JKT Mgambo 3-0, Azam FC 2-0 na Coastal Union 2-0. 
Nyingine zote za kirafiki kama ya leo, Yanga walifungwa 1-0 na Tusker Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kwenda Uturuki, ambako walianza kwa sare ya 1-1 Ariminia Bielefed ya Daraja la Nne Ujerumani, kabla ya kufungwa 2-1 na Denizlispor FC ya Daraja la Kwanza Uturuki na 2-0 na Emmen FC ya Daraja la Kwanza Uholanzi. 


REKODI YA ERNIE BRANDTS YANGA 
Yanga 1-1 Simba SC (Ligi Kuu) 
Yanga 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu) 
Yanga 3-1 Toto African (Ligi Kuu) 
Yanga 3-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu) 
Yanga 3-0 Polisi Moro (Ligi Kuu) 
Yanga 1-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu) 
Yanga 3-0 JKT Mgambo (Ligi Kuu) 
Yanga 2-0 Azam FC (Ligi Kuu) 
Yanga 2-0 Coastal (Ligi Kuu) 
Yanga 0-1 Tusker (Kirafiki) 
Yanga 1-1 Ariminia Bielefed (Kirafiki) 
Yanga SC 1-2 Denizlispor FC (Kirafiki) 
Yanga SC 0-2 Emmen FC (Kirafiki) Yanga SC Vs Black Leopard (Kirafiki)

HAYA NI BAADHI YA MAGAZETI YA LEO NA STORI ZAKE KUBWA.


.

.

.

.


.

.

.

.

.


.

.

Search This Blog