Wanamuziki Fally Ipupa na Ferre Gora kwa pamoja
wamekubaliana kuweka kando tofauti zai za kimuziki na kurekodi wimbo
watakao kuwa wameshirikiana wote.
Kwa mujibu wa muandaaji wa mpango huo Ferre na Fally
watatoa wimbo huo kwa ajili ya kuitakia amani nchi yao. Wimbo huo
utajulikana kwa jina la Congo mon pays (Congo ni nchi yangu). Fally na
Ferre ambao wanatajwa kama ni kizazi cha tano cha muziki wa Congo.
Albamu hiyo ambayo haijasemwa bado itakuwa na nyimbo ngapi lakini
itaachiwa mwezi ujao ambapo DRC Congo itakuwa inaadhimisha miaka 52 ya
Uhuru..
Pichani ni wanamuziki wakiwa kwenye mazoezi ya Wimbo huo. Picha kwa hisani ya Villageafro.com
Awali muandaaji wa project hiyo Brother Patrick Mboyo, alisema kuwa mpango ulikuwa kuwashirikisha wanamuziki kadhaa wa Congo kama Lokua Kanza, Longomba, Olivier Tshimanga Aimelia, Soleil Wanga, Papa Wemba, Felix Wazekwa, Serge Mabiala Celao Scram, etc.. Mpaka sasa Project imeshawakutanisha wanamuziki kadhaa wanaoishi Ufaransa na kwa sasa ndio wanakutanishwa wale wanaoishi Kinshasa.
Aidha Mboyo amesema kuwa wadhamini wakuu wa Project
hii ni Shirika la Msalaba Mwekundu Red Cross na Unicef. Mboyo amesema
haikuwa kazi ndogo kuwakusanya na kuwafanya wote wakubaliane na wazo na
wakubali kufanya kazi pamoja lakini nashukuru tumefanikiwa. “Dhamira
kuu ya Project hii ni kuwakusanya wanamuziki wote wa DRC ili tuijenge
Congo yetu kupitia Music” alisema Mboyo.
“Tunataka kupitia music tuweze kujenga Hospitali,
tuzikarabati nyingine na kujenga mashule, huu ni mpango mpya wa
kuijenga Congo yetu.” aliongeza Mboyo.
Albamu hii itauzwa ulimwenguni kote ambako kuna
mashabiki wa muziki wa Congo na mapato yatapelekwa moja kwa moja Red
Cross na UNICEF. Hii ni kama “We Are The World” ya DR-Congo alimalizia
Mboyo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.