niliwahi kuandika kuhusu huyu mtoto Gloson, Blogger
mdogo toka Malaysia ambaye kwa kiasi kikubwa amejizolea umaarufu
duniani kote kwani pamoja na umri mdogo ameshatunga vitabu viwili vya
mashairi akiwa amenyakua zawadi kadhaa kwenye category yake upande ya
poetry.
hivi karibuni mtoto huyu alijishindia zawadi kemkem
baada ya kuibuka mshindi kwenye shindano la ku Blog kuhusu Territory
ya Malaysia (Blog4FT (Federal Territories) contest!).
Yeye aliandika kuhusu likizo yake kwenye jiji la Kuala Lumpur ikiwa ni hadithi kwa njia ya Picha zaidi(Gonga hapa).
Mimi binafsi navutiwa sana na huyu mtoto Mara ya
kwanza nilipomuona kwa macho yangu ilikuwa wakati wa maadhimisho ya
kampeni ya kitalii ya Visit Malaysia katika jengo la KLCC nchini
Malaysia, na kipindi hicho alikuwa na miaka 10 tu. nilivutiwa sana naye
kwani aliandika poetry nzuri sana kuhusu theme hiyo. Tangu hapo nikawa
mfuasi wa Blog yake.
Dogo ana mengi sana ya kujifunza kutoka kwake kama
Blogger kwani mwenyewe anasema anatumia muda mwingi sana kufanya tafiti
mbali mbali na anapenda sana ku Blog na pia likuwa na kiu ya kujifunza
English kiu ambayo imemfanya awe mtaalamu wa Lugha na kuzawadiwa zawadi
kadhaa kutokana na vitabu vyake alivyoweza kutunga mpaka sasa.
Gloson ameandikwa kwenye vyombo vingi sana vya habari ndani na nje ya Malaysia, Hii yote ni kutambua mchango wake na kipaji chake.
Huu ulikuwa utambulisho wangu miaka miwili iliyopita niliandika kuhusu mtoto huyo kipindi hicho akiwa na miaka 10 tu.
Gloson, 10 Years Old
Jina Gloson kwa Malaysia limekuwa si geni kwenye
vyombo vya habari hasa baada ya kuandikwa sana kw mwaka jana namaanisha
nusu ya mwisho ya mwaka jana.
Gloson ni mtoto wa miak 10 lakini ni Blogger
anayekuja kwa kasi akiwa na miezi si zaidi ya saba kwenye ulimwengu huu
wa magazeti tando, Kipaji chake si tu kwa kublog bali ni uwezo mkubwa
alionao wa kujieleza, mara ya kwanza nilisoma kwenye gazeti la The Star
haikuniingia hadi nilipoona akihojiwa kwenye Chanel kubwa ya Tv3 na
kumuona kwa macho yangu.
Dogo anakipaji kweli kweli na ye anasema ana blog
kila kitu anachoona kina manufaa kwa jamii na katika blog yake pia
amefundisha jinsi ya kuandika Post yenye mvuto na jinsi ya kuchangia
topic bila kwenda nje ya mada, akiwa ni wanafunzi wa shule ya msingi
Gloson anasema alipata wazo la Ku blog toka kwa mama yake ambaye
alimshauri ablog naye akaanza.
Mbali na kipaji hicho pia Gloson anakipaji cha
kuandika mashairi akiwa meshaandika zaidi ya mashairi 100 ambayo
yamechapishwa www.poetrytalents.com
Ikiwa ni miezi 6 tu tangu ianzishwe blog ya Gloson ambayo inakwenda kwa anuani ya http://www.glosonblog.com/
“Nafurahi ninapo share nilichojifunza na wenzangu”
“naamini nina mchango kwa jamii mengi waweza
kujifunza toka kwangu na kuelimika, kuna mengi yakujifunza kwenye
mtandao, napenda Internet naweza kufanya kila kitu kuanzia Homework,
games, kununua vitu na kuwasiliana na vitu, alisema Gloson alipohojiwa
kwenye Tv3. “kuna vitu siwezi kuwaeleza wazazi wangu moja kwa moja
lakini huwa natuma email na naenda kulala nikiamka baba atanijibu ama
kwa email au hata akikaa kimya najua anatafakari na amepata ujumbe
wangu” aliongeza mtoto huyu anayejua kujieleza kwa lugha ya ufasaha na
kufanya wtangazaji wote kucheka.
Pamoja na vipaji hivyo pia Gloson anakipaji cha
kutumia Photoshop kwa ajili ya kucheza na picha, na ni mtundu wa mambo
ya mtandao pia.
Si mbaya mtembelee hapa utakuta mengi sana ya kujifunza toka kwake. Wana Blog wenzangu mpooo!!!!?
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.