Saturday

MAUAJI YA KINYAMA YATOKEA ARUSHA

Pichani: Mkuu wa mkoa wa Arusha (kushoto) Bw. Magessa Mulongo na maafisa wengine wakiiangalia miili ya watu wanne waliouawa kinyama na kutupwa katika maeneo tofauti ya Kitongoji cha Chekereni wilayani meru wiki iliyopita.

Polisi mkoani Arusha wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mauaji ya kutisha ya watu wanne yaliyotokea juzi katika maeneo tofauti ya kitongoji cha chekereni wilayani Arumeru. imeripotiwa kuwa miili ya watu wote hao wanne imekutwa ikiwa na majeraha makubwa hali inayodhihirisha kuwa waliteswa ama kupambana kabla ya mauaji hayo kutokea, wawili kati yao wamekutwa wakiwa wamefungwa na minyororo mikononi.
Mnamo Aprili 21 Maiti ya vijana hao wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 35 ilianikwa nje ya hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kutambuliwa ambapo mamia ya watu walijitokeza weng wakionesha wazi kushangazwa na ukatili wa aina hii. Maiti za vijana hao iliweza kutambulika kwa majina Laizer Nalaba mkazi wa Mbauda, Jumbe Saitoti mkazi wa Sokon 1, Elias Loiting'idaki wa Sombetini na Richard Maombi maarufu kwa jina la Boshuu ambaye pia ni mkazi wa Sombetini. taarifa zaidi kutoka kwa polisi zinadai kuwa kuna uwezekano kuwa watu hawa wameuawa katika eneo moja mkoani Arusha na kwenda kutupwa katika maeneo mbalimbali ili kupoteza ushahidi. Kuthibitisha hili polisi wamedai kuwa kuna umbali angalau wa kilomita mbili kutoka mahali miili ile ilipokuwa imetapakaa na pia majeraha yanaonesha kuwa ya aina moja.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha ameripoti kuwa tarehe 21 Aprili walipokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema zikiwataarifu kuwa kuna maiti imeonekana pembezoni mwa barabara mkabala na shule ya sekondari Tengeru boys na wakati wakielekea katika eneo la tukio walipata habari zingine kuwakuna maiti zingine zimeonekana karibu na mto Nduruma na nyingine katika eneo la mto Oraki katika kijiji cha Nambala wilayani Arumeru mkoani Arusha.

hadi habari zinatufikia, taarifa zinasema kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi na haijaweza kufahamika mara moja kuwa ni nani waliohusika na mauaji hayo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog