Monday

JK AIONGOZA KAMATI KUU WHITE HOUSE




Rais Jakaya Kikwete (wa kwanza kulia) akiongoza kikao cha kamati kuu ya CCM leo Ikulu. Picha na Ikulu.

JK AWASILI TANGA KUSHEHEREKEA MEI MOSI KESHO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa ka furaha na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyaakzi Tanzania (TUCTA) Bw Nicholaus Mgaya  leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi

Sunday

Rais wa Malawi amfuta kazi hasimu wake

Rais mpya wa Malawi Joyce Banda amemfuta kazi Waziri wa mambo ya nje Peter Mutharika, kakake Marehemu Rais Bingu Wa Mutharika aliyefariki dunia mwezi huu.

Mutharika alitarajiwa kurithi Marehemu Kakake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2014 ambapo Bingu Wa Mutharika alitarajiwa kustaafu.
Mabadiliko ya baraza la mawaziri yametokea siku chache baada ya maziko ya Rais huyo mapema wiki hii. Bi. Banda amekuwa Makamu wa Rais tangu mwaka 2009 lakini akatofautiana na Wa Mutharika na kuwa mksoaji wake mkubwa.
Kufuatia kifo cha Rais huyo kulizuka wasi wasi kwamba wandani wake wangejaribu kuzuia ukabidhi wa madaraka kwa Bi. Banda ambaye alikuwa na chama chake cha kisiasa.
Miongoni mwa Mawaziri wapya ni Austin Atupele Muluzi, mwanawe Rais wa zamani Bakili Muluzi aliyeteuliwa Waziri wa mipango na ustawi.Wengi waliotimuliwa na waliokuwa wandani wa Bingu Wa Mutharika.

Kanisa lashambuliwa Nairobi

29 Aprili, 2012 - Saa 08:51 GMT

Mlipuko kwenye kanisa mjini Nairobi, Kenya, umeuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine 10.
Polisi wanasema guruneti lilirushwa kwenye kanisa la God's House of Miracle kwenye mtaa wa Ngara, wakati wa ibada ya asubuhi.

Daktari mmoja katika Guru Nanak Hospital mjini Nairobi, ambako ndiko majeruhi walikopelekwa, aliwaelezea waandishi wa habari majeruhi aliowaona:

"Tumepokea majeruhi 7, mwanamke mmoja aliumia vibaya kwenye mguu wa kushoto, ambao umevunjika mahala kadha.

Mwanamme mmoja alikuwa na majaraha kadha kwenye nyama na tunafikiri amevunja mifupa piya; labda tukimfanyia x-ray tutatambua.

Kuna mama mmoja aliyevunja kidogo kisuguru cha mguu wa kushoto, na wengineo wamepata mikwaruzo-kwaruzo na kujikata-kata."

Kumetokea mashambulio kadha ya maguruneti nchini Kenya tangu mwaka jana pale serikali ilipotuma wanajeshi Somalia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu, Al-Shabaab.

Search This Blog