Monday

PICHA 11 ZA DIAMOND PLATNUMS AKIWA MAREKANI, PIA JINSI ALIVYOPOKELEWA.




Diamond Platnums akiwa Washington Marekani na dancers wake, hii ni kwa mwaliko wa kuperform kwenye ardhi ya Obama.

.

.

.

.

.

Jinsi alivyopokelewa….

.

.

Picha zote ni kutoka kwenye website yake
.

Wema Sepetu BIOGRAPHY


 Early Life
Wema hails from a Diplomat Family ; the last child in a family of four girls of Ambassador Isaack Abraham Sepetu. This beautiful soft spoken and light skinned girl, started performing since her childhood in school Drama’s in Dar es Salaam. She was born in 1988 at Dr Andrew’s Hospital, Dar es Salaam.
'Wema' means Kindness in Swahili.

Education
Wema completed her primary and secondary education in Dar es Salaam at Academic International. She went for International Business course at Limkokwing University, Malaysia.

Career
Wema burst into the Tanzania film industry with the movie Point Of No Return, in 2007 where she played as a wife of a rich witch guy who always killed his girlfriends for sacrifice. Wema thought she would die too but, she decided to pray and at last saves her husbands family and herself. This film received good reviews on film industry.
Wema has starred in Tanzania Film Industry with movies like Red Valentine, White Maria, Tafrani, Sakata, Crazy Tenant, Diary, Lerato, Dj Benny and Basilisa. 

Beauty
In 2006, she was crowned as Miss Tanzania, the competition which was held at Diamond Jubilee Hall in Dar es Salaam. More than 20 girls compete from 25 regions of Tanzania. She was awarded a Toyota Rav 4 and a ticket to compete in Miss World.
Wema also can sing.

Philosophy: Don’t Give Up
Music: R n’ B
Hair Style: Anything sexy
What she admires about people: True Love
Attractiveness in a guy: Smartness
  Favorite Color: Purple and Orange
 
For more info visit my website

KAMA ULIKOSA UZINDUZI WA ALBAMU YA PASCAL CASIAN WA BSS,"YASAMEHE BURE" TWENDE PAMOJA PICHANI



Madam Ritha akisindikizwa kuelekea jukwaani



Wanafamilia na watoto mbalimbali pia walijitokeza kuchangia siku hiyo



akiinadi albamu hiyo yenye picha yake nyuma



akikata utepe kuzindua



Katika picha ya pamoja na Paschal



Mdam Rita akichangisha fedha za kwa ajili ya huduma ya kuwasaidia machangudoa wa Uwanja wa Fisi



Paschal akiimba huku akicheza



wadau mbalimbali walijitokeza kununua albamu hiyo



umati mkubwa wa watu ulihudhuria

TANZANIA YANGU NA MAKABILA YAKE NA UTAMADUNI WAKE..WAGOGO TOKA DODOMA.!!!

Tanzania ni nchi ambaye ina makabila mengi sana zaidi ya 130..Na kila kabila lina mila na utamaduni wake. Binafsi najivuna sana kuwa mtanzania leo tuwatembelee wenzetu wagogo kwa mtindo wa kuwasikiliza wakiwa wakiimba na kucheza..
       
          

TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF)KWA VYOBO VYA HABARI KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI



UTANGULIZI:

1. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwandishi wahabari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.

2. Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini jana, Septemba 2, 2012, wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

3. Tukio hili linaiingiza Tanzania katika historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wahabari, kwani ni kwa mara ya kwanza tunashuhudia mwandishi wa habari AKIUAWA WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIHABARI.

4. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti saa 9.30 alasiri katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio. Na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.

5. Kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania, TEF tumechukua hatua za haraka za kuunda timu ya uchunguzi wa suala hilo, ambayo itakwenda mkoani Iringa mapema kadri itakavyowezekana, ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Lengo la uchunguzi huo ni kuweka kumbukumbu sahihi (documentation) ya tukio hilo la aina yake katika historia ya nchi yetu.

6. Matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mwingine unaofanywa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa hatua ambazo TEF inachukua dhidi ya Jeshi la Polisi katika siku chache zijazo.

MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF

Kwa kuzingatia taarifa kutoka Iringa na zile za vyombo vya habari vya jana (Jumapili, Septemba 02, 2012) na leo (Jumatatu, Septemba 03, 2012), TEF ina mtizamo na msimamo kama ifuatavyo:

1. Kwanza tunalaani vikali tukio la kupigwa, kisha kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosiambalo limeigusa tasnia ya habari kwamba sasa pengine waandishi wa habari ni malengo “target ya polisi” wanapokuwa kwenye kazi zao.

2. Ieleweke wazi kwamba matukio haya siyo yanaondoa imani ya waandishi wa habari kwa jeshi lapolisi tu, bali yanaweza kuwa chanzo cha uhasama na ufa mkubwa ambao utawanyima wananchi nafasi ya kutumikiwa na pande mbili ambazo zinategemeana.

3. Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.

4. Tunasema hivi kwani kuna kila dalili kwamba polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine na tukio au/na matukio yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, kwani kitendo cha kumzingira tu na kumshambulia kinathibitisha kwamba hawakuwa na nia njema hata kidogo dhidi ya mwandishi huyu.

5. Taarifa ambazo TEF tunazo, pia zinadai kwamba kulikuwa na mpango wa polisi wa “kuwashughulikia waandishi wa habari watatu” (Mwangosi) akiwa mmojawapo na hilo lilionekana likitekelezwa kwa polisi kumshambulia mwandishi huyo, baadaye alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.

6. Hili linatiliwa nguvu na tukio jingine la polisi kumpiga na kumjeruhi mwandishi mwingine, Godfrey Mushi ambaye ni mwakilishi wa gazeti la Nipashe mkoani Iringa. Mwandishi wa tatu ambaye hadi tunapoandika taarifa hiyo yumo katika mpango wa ‘kushughulikiwa na polisi’ ni Francis Godwin ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.

7. Vitendo vya aina hii havivumiliki na havipaswi kuachwa kuendelea kwani ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na uhuru wa habari nchini. Hatuwezi kuendelea katika mazingira ambayo polisi wanageuka kuwa chombo cha mauaji ya raia badala ya kuwa walinzi wa raia.

8. Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.

9. Mwenendo wa aina hii wa chombo cha dola kuamua kutumia silaha kuua na baadaye kupanga mbinu chafu za kuficha ukweli ni hatari kwa Taifa, na unaiweka demokraisia ya nchi yetu njia panda, huku tukielekea katika hatari ya Taifa kutumbukia katika uovu.
IMETOLEWA NA:
NEVILLE MEENA,
KATIBU MKUU – JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)

Search This Blog