Saturday

MANENO ALIYOZUNGUMZA TAMEKA RAYMOND KWA MARA YA KWANZA TOKA UTOKEEE MSIBA WA MWANAE NDIO HAYA.


                                        Marehemu Kile na mama mzazi Tameka.

Zikiwa hata wiki mbili hazijaisha toka mke wa zamani wa mwimbaji Usher Raymond Tameka Raymond kumzika mwanae kipenzi Kile aliefariki dunia kwenye ajali iliyotokana na pikipiki zinazoendeshwa kwenye maji, Mama huyu wa watoto watano ametoa kauli ya kwanza toka msiba utokee.

Tameka ambae kwa kipindi kirefu amekua mahakamani kutokana na kesi ya kugawana watoto yeye na mumewe wa zamani Usher Raymond, amesema hii statement haijaandikwa na timu yake, msaidizi wake wala yeyote bali ni maneno ambayo ameyaandika kutoka moyoni mwake.

Ripoti yake inasema hivi “Kwa majonzi makubwa nimejikuta nikilazimika kujibu waraka wa mahakama unaonitaka nifike Mahakamani kwenye kesi ambayo sio mimi niliyeianzisha, sikumshitaki mtu yeyote kwenye hii kesi ya January 2011 japo niliridhika na maamuzi ya ya kugawana majukumu kuwalea watoto”


.

“Kinachonisikitisha ni kulazimika kwenda Mahakamani katika kipindi ambacho naomboleza kifo cha mwanangu, hata hivyo sitozuia Mahakama kufanya kazi yake, nitaendelea na yale yote nitakayolazimika kuyafanya huku nikiwa na matumaini kuwa hali hii ngumu itanisaidia kupambana na hali nyingine ngumu zaidi ya majonzi ya mwanangu” – Tameka

Kwenye line ya mwisho, Tameka mwenye umri wa miaka 41 amesema “naisihi jamii yote kutoamini yale yote yanayosikika kwenye vyombo vya habari na pia jamii isiwe nyepesi ya kuhukumu, wanangu ndio ulimwengu wangu na nitapambana kufa na kupona kuwalinda na kuwa nao maisha yangu yote”

Hiyo ni taarifa kupitia mtandao wa Global Grind, Hallo Beautiful wameripoti kwamba Usher Raymond hakutoa ushirikiano wowote kipindi cha msiba na hakuwahi kuongea na Tameka wala familia yake, pia alikwenda kumzika Kile kwa sababu tu tayari anajulikana kwamba ni mtoto wake wa kufikia na vyombo vya habari na watu wengine walitegemea kuona angefanyaje kwenye maziko ya mtoto wa mke wake wa zamani.

HBL wameripoti zaidi kwamba taarifa zilizopo ni kwamba wakati wote wa msiba Usher alikua hapokei simu za Tameka wakati alipohitajika kutoa msaada wa pesa kwa ajili ya matibabu ya Kile alipokua kalazwa.

HILI NDIO JUMBA WALILOLIKODI JAY Z NA BEYONCE KWA MAMIA YA MAMILIONI KWA MWEZI.




Fahamu kwamba wamefanya hivi sio kwa sababu wana uhaba wa nyumba, yani pamoja na kumiliki majumba kadhaa ya kifahari lakini wameamua kulikodi hili jumba pia ambapo wanalilipia dola za kimarekani laki nne kila mwezi ambazo kibongobongo ni zaidi ya Milioni 600.

Moja kati ya vitu vilivyowavutia kukodi hili jumba huko Bridgehampton New York Marekani ni pamoja na ukaribu wake na bahari, ni nyumba ambayo wameikodi kwa mwezi mmoja tu wa August according to New York Daily News, lakini nyumba yenyewe pia inauzwa kwa USD 43 million.

Ukiishi kwenye hii nyumba unapata 60-foot pool, a two-lane bowling alley; tennis , squash, racquetball and basketball courts and a children’s performing area.


.


.


.


.


.


.\


.

BREAKING NEWS: ROMA APATA AJALI MBAYA NA GARI, USHAHIDI WA PICHA HUU HAPA.



.
Stori ni kwamba msanii wa Bongo fleva Roma Mkatoliki amepata ajali mbaya ya gari Morogoro road ambapo kwa mujibu wa djchoka.blogspot.com ni kwamba tairi la mbele lilipopasuka na gari likaacha njia na kugongana uso kwa uso na fuso ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha Roma kurudi lilipotokea.

Roma amemuambia Dj Choka kwamba anaelekea hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye gari hakuna aliyeumia wote ni wazima.

Roma amepata ajali hii leo ikiwa ni siku 18 tu toka msanii mwingine wa bongofleva Chege kupata ajali ya gari yake kwa kumgonga mtu wa pikipiki alieingia barabarani ghafla na kusababisha gari kuharibika.


.


.


.


.


.


Picha zote zimetoka kwa djchoka.blogspot.com

Friday

ANDRE 3000 KUDIRECT VIDEO 16 KUTOKA KATIKA ALBUM YA GOD FORGIVES, I DON’T YA ROZAY.




Mkali aliyerikishwa kwenye ngoma ya Green light ya John Legend member wa OutKast akadrop bars za ukweli  homie Andre 3000 sio tu kwamba amealikwa auzee sura kwenye video!!  no pia anadirect video 16 za Bawse Rozay  kutoka kwenye album ya “God Forgives, I don’t”
“3000 kwa sasa bado anaongezea mawazo mapya kwenye video hizo ili aweze kufanya video kali” alisema Rozay  ambae ni Boss wa Maybach Music wakati akipiga stories na MTV News kwenye RapFix Live Jumatano iliyopita.
Rozay mpaka sasa ameshaachia ngoma nne kutoka kwenye album hiyo na anayo mipango ya kuachia nyingine zaidi. Atafanya video za ngoma zote ambazo zinapatikana kwenye album yake.

BEYONCE KUSHOOT VIDEO YA WIMBO WAKE WA "I WAS HERE" SIKU YA WORLD HUMANITARIAN DAY.





Mwanadadiva mwenye mtoto mmoja muite mama Ivy mke wa mkali wa kwenye ngoma ya Ortis Jay z akiwa na Boss wa Good Music Kanye West mwanamama Beyonce, amejitolea sauti yake iliyobarikiwa kwenye kitu cha maana. Beyonce ametangaza kufanya video ya ngoma ya “I was Here” kwa heshima ya World Humanitarian Day, siku hiyo wakati akiperform watu watakaoonekana ndo itaonekana kwenye video yake hiyo.
 Diva huyo amejiunga na shirika la United Nations & Humanitarian Aid Organization kwa ajili ya kuzindua kampeni ya kusherekea kazi za kujitolea zinazofanywa na watu mbalimbali na kuwapa moyo watu duniani kote kufanya mambo mema kwa watu wengine ambao wako kwenye matatizo. Video itafanywa na kampuni ya Ridley Scott & Associate na madirectors wakali kama Kenzo Digital na Sophie Muller. Kampeni hiyo inalengo la kufikia watu bilioni 1 na ujumbe mmoja wakati wa uzinduzi siku hiyo

HIKI NDICHO KIPYA ALICHOSEMA JAGUAR KUHUSU KUMSUPPORT PREZZO KWENYE BIG BROTHER.


Jaguar.

Juzi Aug 1 2012 stori kubwa ya Jaguar kumdiss Prezzo kwenye page yake ya mtandao wa kijamii wa twitter kwamba Wakenya na Waafrika wengine wasimpigie kura kwa sababu hatakiwi kushinda hizo pesa za Big Brother ndio iliibuka.

Kila alieona hizo tweets alishtuka manake zilikua na maneno mazito na zilikua zinachana waziwazi.

Baada ya watu wengi kuamini kwamba ile account ni ya Jaguar, ameongea Exclusive na millardayo.com na kusema kwamba hana account ya twitter.

Amesema “nimeshtuka sana na nimepigiwa simu nyingi lakini sina account ya twitter, niko facebook tu na siku zote nimekua nikisema tumpigie kura Prezzo tumsupport kama Mkenya mwenzetu, namsupport kabisa kama kaka yangu kwa sababu zile hela hata zikienda kwa mtu mwingine labda Zambia au South Africa hazinisaidii, afadhali zichukuliwe na Mkenya mwenzangu”

Baada ya kuyasema hayo, Jaguar akamalizia kwa kutamka “tofauti zetu ni za muziki lakini sio yeye kwenda Big Brother, namsupport kwenda Big brother kwa sababu anahitaji hizo pesa sana sasa akizipata ndio aje tuonane, hata hivyo haitakua kitu kikubwa sana akishinda hizo milioni 24 japo itakua vizuri kwa sababu ndio tutaweza kukaa kama wanaume manake kipindi cha nyuma hatukuweza kwa sababu hakuwa na pesa, ndio maana namsupport sana sasa hivi ili nisikie ataongeaje akiwa na pesa kwa mfuko”

Jaguar na Prezzo bado wako kwenye beef ambayo ilianza longtime kidogo kwa Jaguar kusema kwamba Prezzo hawezi muziki na ishu zake za kujisifia mavazi na bling bling zimeshapitwa na wakati, pesa anazoringia ni za wazazi lakini yeye (Jaguar) pesa zake ni za jasho lake.















.

MJUSI ANAEFANANA NA SPIDER MAN



Mjusi huyu alipigwa picha hapa hapa Afrika na kuibua maswali inakuwaje kuwaje anafanana na vazi analovaa spider man wa kwenye movie??




Mjusi huyu alipigwa picha na wanandoa kutoka Sao Paul Brazil ambao ni Mr. & Mrs.Cassio Lopez.


Wakiwa Masai Mara naional park katika mto Rongai nchini Kenya ndio walimuona mjusi huyo akipita wakampiga picha.

HUU NDIO USHAHIDI WA PICHA WA MRISHO NGASA KUANZA MAZOEZI NA SIMBA, NA HILI NDIO GARI ALILOPEWA PIA.

Hili ndio gari jipya la Mrisho Ngasa alilopewa kwenye huo uhamisho wa kuingia Simba kwa mkopo akiwa anaingia nalo kwenye mazoezi na Simba leo.
Mrisho Ngasa ni baba wa watoto watatu katika ndoa aliyofunga miaka minne iliyopita.
Ngasa akiwa anaingia kwenye mazoezi Coco beach na club yake mpya ya Simba.
Leo ndio Mrisho Ngasa ameanza mazoezi na Simba leo.
.
Salute kwa Saleh Ally wa gazeti la Champion kwa kunitumia hizi picha.
Jinsi Mrisho Ngasa alivyopokewa na mashabiki wa Simba kwenye makao makuu ya club hiyo.
Jana Club ya soka ya Azam ilitangaza kwamba Mchezaji wao Mrisho Ngasa tayari amepelekwa Simba kwa mkopo ambapo Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) kwa mwezi pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba.
Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki Azam Fc, Pia iliwekwa wazi kwamba Azam haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa, Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC.
Azam ilisema “Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu, Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipotayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu”
Azam ilisema kosa alilolifanya Ngasa ni kubusu na kuvaa jezi ya Yanga wakati bado ni mchezaji wa Azam hivyo ilionekana ni kitendo cha nidhamu mbovu na kuidhalilisha brand ya Azam

Search This Blog