Saturday

MITANDAO YACHANGIA ONGEZEKO LA KASI YA UKAHABA VYUONI (UDSM) (UDOM) (CBE) (IFM)(SAUTI)


 Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo. Imefahamika kuwa Baadhi ya wanafunzi wanatumia mitandao ya kijamii katika kufanikisha biashara ya ngono. PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi.
Uchunguzi umebaini kuwa matumizi mabaya ya teknolojia hasa mitandao ya kijamii yamechochea ongezeko la uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya na zaidi biashara ya ukahaba vyuoni.
Mitandao ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa namna inavyoweza kuwaunganisha watu kutokana na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga mitandao ya kibishara, kidini, michezo, burudani, vichekesho na mengine ambayo mara nyingi huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na kuona kinachoendelea ndani.
Mbali na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi yanayoendesha biashara ya ukahaba, yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini kwa kupitia kurasa mbalimbali kama vile ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyinginezo.

Uchunguzi umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kutumia mitandao wameweka picha na namba kwa ajili ya mawasiliano kwa mteja atakayekubaliana na bei waliyoweka.

Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia katika mitandao ya Facebook, Twitter, BBM, Instagram, utabaini kuwapo kwa makundi yaliyoundwa kutengeneza mitandao ya ngono, ambayo huweka pia namba za simu za wahusika, zikiambatana na picha, ambao ikiwa utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza ukapiga simu husika kuzungumza naye kwa kufanya mapatano kabla ya kukubaliana.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao hiyo. 
Baadhi ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na kujitangaza kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Kwa nyakati tofauti, waandishi wa gazeti la Mwananchi walitembelea makundi yanayojinadi kufanya biashara hiyo pamoja na kufanya mawasiliano na wasichana watatu ambao waliweka picha na namba zao kwenye mtandao

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog