Friday

KUHUSU JAMIE FOXX KUKATAA KUKUTANA NA BABA YAKE MZAZI.

On Streets Today
         

Jamie Foxx.

Stori kutoka the Box ni kwamba movie star ambae ni mwimbaji pia Jamie Foxx amekataa kabisa kuonana na baba yake mzazi ambae ni mgonjwa kwa sasa.

Sababu pekee inayofanya Jamie asitake kuonana wala kumsamehe baba yake ambae ana umri wa miaka 74 ni kutokana na mzazi huyo kumtelekeza akiwa mdogo.

Jamie alilelewa na bibi yake ambae alifariki mwaka 2004, toka mwaka huo Jamie hajawahi kuongea na baba yake mzazi.

Kwa sasa baba yake mzazi ni mgonjwa sana na amekua akihitaji kuonana na Jamie ili wayamaliza lakini staa huyu amekataa.

Mke wa sasa wa baba yake Jamie amekaririwa akisema “tumekua tukimpigia simu Jamie kwa miaka sasa lakini hapokei na wala hajawahi kujibu mamia ya msg tulizomuandikia, na sasa baba yake ni mgonjwa na anapumulia mashine… natamani Jamie apige simu”

Ni mastaa wengi wa dunia mpaka sasa ambao wamekua kwenye uhusiano mbaya na baba zao akiwemo Beyonce, Kelly Rowland nae alikua haongei na baba yake, movie star Angelina Jolie mpaka sasa bado hayuko kwenye uhusiano mzuri na baba mzazi.

UNAAMBIWA HILI NDIO GARI ANAMILIKI VIDEO QUEEN WA YOU GUY YA P UNIT KENYA

On Streets Today





Kwa mujibu wa mtandao wa Ghafla Kenya, yule mrembo alieng’aa kwenye video ya single mpya ya P Unit (You Guy) ambayo imefungiwa na kituo cha CITIZEN TV aitwae Vee Beiby anamiliki huu mkoko hapa, BMW Z3 Roadster.

Unaweza kumchek kwenye interview hapa chini na pia kwenye hiyo video ya P Unit chini yake.

                       


Video ya mwisho ni behind the scene ya wakati video ya ‘You guy’ ikitengenezwa.

TAARIFA KUHUSU DHAMANA YA MWIGIZAJI LULU AMBAYO ILIKUA ITOKE LEO.


On Streets Today

Elizabeth Michael. Jana kwenye allstreetsonline.com kulikua na stori kwamba uwezekano wa mwigizaji Lulu kuachiwa kwa dhamana january 25 2013 ulikuepo.


Ni kweli ilikua iwe hivyo lakini kwa taarifa zilizotolewa na vyombo husika ni kwamba dhamana hiyo imeshindikana kutolewa leo.


Sababu kubwa ni leo kuwa sikukuu hivyo shughuli imesogezwa mbele mpaka jumatatu january 28 2013.


Mwanzoni Lulu ambae anatuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia ilidaiwa alikua anatakiwa apate dhamana ambayo milioni 20 zilihitajika (kwa mujibu wa taarifa za ndani) ila ikashindika sababu jaji alipata udhuru.


Lulu amekua chini ya ulinzi toka kifo cha mwigizaji staa wa movie Tanzania Steven Kanumba April 2012.

ISOME TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA JAN 25 IKO HAPA

On Streets Today
WILAYA YA MOMBA – KUVUNJA CHUMBA CHA GUEST MCHANA NA KUIBA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani

MNAMO TAREHE 24.01.2013 MAJIRA YA SAA 10:30HRS HUKO KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO SERENGETI ILIYOPO TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. JOYCE D/O KEMTO,MIAKA 38,MFANYABIASHARA,MKISII MKAZI NA RAIA WA NCHINI KENYA ALIYEKUWA AMEPANGA KATIKA CHUMBA NO.06 ALIIBIWA PESA TSHS 150,000/= ZILIZOKUWA KWENYE MKOBA NDANI YA CHUMBA HICHO. WATUHUMIWA WAWILI 1.EMANUEL S/O CHARLES, MIAKA 40, MZANAKI, MKULIMA MKAZI WA MAGOMENI DSM NA 2. GODFREY S/O BENARD @ SIMFUKWE,MIAKA 42,MUHA,MKULIMA MKAZI WA MWANDIGA KIGOMA WAMEKAMATWA WAKIWA NA MKOBA WENYE PESA HIZO. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUPANGA CHUMBA JIRANI NA MHANGA NA KISHA KUFUNGUA MLANGO WA CHUMBA KWA KUTUMIA FUNGUO BANDIA WAKATI MHANGA AKIWA NJE. MHAMGA ALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA BAADA YA KUWAONA WATUHUMIWA WAKIWA NA MKOBA WAKE NA NDIPO WANANCHI WALIPOANZA KUWASHAMBULIA KWA KUWAPIGA MAWE NA FIMBO HATA HIVYO WALITOKEA ASKARI POLISI NA KUWAOKOA. MTUHUMIWA GODFREY S/O BENARD @ SIMFUKWE HALI YAKE NI MBAYA AMELAZWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA NA MWENZAKE ANAENDELEA KUSHIKILIWA POLISI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA PINDI WANAPOWAKAMATA WAHALIFU NA BADALA YAKE KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE. AIDHA ANATOA RAI KWA WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI KUIMARISHA ULINZI MUDA WOTE KATIKA BIASHARA ZAO. PIA ANAWAKUMBUSHA KUTOA TAARIFA HARAKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILISHA SHAKA AMBAO WANAFIKA KAMA WATEJA ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.

WILAYA YA KYELA – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MNAMO TAREHE 23.01.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IBANDA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. POLISI WALIWAKAMATA WATU WATANO RAIA WA NCHINI BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI AMBAO NI {1}.ALAKEZA S/O MOSE,MIAKA 32 {2}. BULALAHUBWA S/O KALODATI, MIAKA 25 {3}. ALAKAZYA S/O ALINI, MIAKA 6 {4}. NISHUNA D/O DORINA, MIAKA 6, NA {5}. MUNYEZE D/O JOZINA, MIAKA 9 . MBINU ILIYOTUMIKA NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO NA KUKUTWA KATIKA KANISA LA BABTISTI KIJIJINI HAPO WAKIOMBA HIFADHI. WATUHUMIWA WAMEKABIDHIWA IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KWA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU.

WILAYA YA MBOZI – KUSALIMISHWA KWA SILAHA MOJA AINA YA GOBOLE

MNAMO TAREHE 23.01.2013 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IYULA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. MTU/WATU WASIOFAHAMIKA WALISALIMISHA /TELEKEZA BUNDUKI MOJA AINA YA GOBOLE YENYE NAMBA – TOWKK 340. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUTELEKEZA SILAHA HIYO JIRANI NA KITUO KIDOGO CHA POLISI IYULA NA POLISI KUICHUKUA . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWAFICHUA KWA KUTOA TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAOMILIKI /TENGENEZA SILAHA BILA KIBALI ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANATAHADHARISHA WAMILIKI/WATENGENEZAJI HARAMU WA SILAHA HIZO KUZISALIMISHA HARAKA INGAWA MUDA WA “OFFER” UMEMALIZIKA KULIKO KUSUBIRI KUKAMATWA.

WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 24.01.2013 MAJIRA YA SAA 18:56HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NZIGWA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1.MAKENZA S/O IGEMBE, MIAKA 45, MSUKUMA, MKULIMA NA 2. MILEMBE D/O MALA,MIAKA 65,MSUKUMA MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA NZIGWA WAKIWA WANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA NUSU EKARI . WATUHUMIWA NI WAKULIMA NA WAUZAJI WA BHANGI. BHANGI YOTE IMETEKETEZWA KWA KUCHOMWA MOTO SHAMBANI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WAMILIKI NA MAHALI YALIPO MASHAMBA YA BHANGI KUZITOA KWA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA DHIDI YA WAHUSIKA ZICHUKULIWE.

Signed By,

[DIWANI ATHUMANI – ACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Thursday

PICHA NA TAARIFA ZA VURUGU ZINAZOENDELEA KIBITI RUFIJI SASA HIVI, WANANCHI WAMEVAMIA POLISI.. WANACHOMA

On Streets Today

Mwandishi Mrokim waFather Kidevu Bloganaripoti kwamba kundi la wananchi wenye hasira wamevamia kituo cha Polisi Kibiti Wilayani Rufiji na kuleta vurugu kubwa kutokana na raia mmoja kufa kwa kile kilichodaiwa kuwa kipigo cha Polisi.
Aliyefariki ni Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Muhimbili.

Habari za sasa ni kwamba wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari Polisi zilizopo jirani na kituo hicho licha ya juhudi za Polisi kuwatawanya kwa mabomu, pia wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti, hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya watu.

LULU KUACHIWA KWA DHAMANA.

On Streets Today



Taarifa za uhakika nilizozipata kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Lulu akatoka kwa dhamana kesho january 25 2013.

Uhakika wa Lulu kupata dhamana ulikua jana jumatano january 23 lakini ikawa imeshindikana kutokana na kuahirishwa kwa sababu jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua hakijatimia.

Chanzo cha kuaminika kilichoongea na millardayo.com kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.

Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba, endelea kuipitia millardayo.com kwa stori zaidi.

Search This Blog