Sunday

Zimbabwe yapiga kura ya maoni ya katiba

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekanusha malalamiko kwamba wananchi hawakuelezewa ipasavyo kuhusu katiba mpya.

Bwana Mugabe aliiambia BBC kwamba Wazimbabwe walishauriwa sana kuhusu katiba hiyo na walitoa maoni yao.

Kura ya maoni kuhusu katiba mpya inafanywa nchini Zimbabwe leo.

Chama cha Rais Mugabe cha Zanu-PF na kile cha MDC cha Morgan Tsvangirai ambacho kimo kwenye serikali ya mseto, vinaunga mkono katiba mpya.

Waandishi wa habari wanasema wakati wa kampeni pamekuwa na mvutano nchini Zimbabwe kabla ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanywa baadae mwaka huu.

Vyama vikuu vya Zimbabwe vina msimamo mmoja kuhusu katiba inayopendekezwa.
Vinaiunga mkono.

Inavoelekea katiba itakubaliwa na wengi lakini inawezekana wataojitokeza kupiga kura ya maoni ni wachache.
Katiba hiyo ni muhimu kuielekeza nchi kwenye uchaguzi huru na wa haki.
Ina vipengee vya haki za wananchi na vizuizi dhidi ya madaraka ya rais mtendaji.
La kutatanisha ni kuwa katiba mpya inataka rais atumike kwa mihula miwili ambayo itampa Rais Mugabe, mwenye umri wa miaka 89, uwezekano wa kuongoza kwa miaka kumi zaidi

PAPA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI

Papa Francis aliyechaguliwa hivi karibuni, amekutana na waandishi wa habari mjini Rome akisema kuwa atapenda kanisa maskini lenye lengo la kuwasaidia maskini.
Katika hatua ambayo Vatikani imesema inaonesha uwazi zaidi, Papa mpya alizungumza na mamia ya waandishi wa habari na alisema alichagua jina la Mtakatifu Francis wa Assisi kwa sababu alikuwa mtakatifu wa amani, matumizi haba na kutumikia maskini

"Wakati wa uchaguzi wa papa mpya kando yangu alikuwa Askofu wa Sao Paulo, Claudio Hummes.

Ukweli ulipokuwa unakaraibia alinipoza.

Na kura zilipotimia thuluthi mbili alinikumbatia na kunibusu.

Aliniambia "usiwasahau masikini".

Na hilo limebaki nami...masikini, masikini

Search This Blog