Friday

ZANZIBAR YATAKA USHIRIKIANO ZAIDI NA CUBA KATIKA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliuongoza
Ujumbe wa Zanzibar katika Kikao cha pamoja na Ujumbe wa Wizara ya
Biashara za  Nje na Uwekezaji wa Cuba ulioongozwa na Waziri wake Bwana
Rodrigo Malmierca Diaz. Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya Wizara
hiyo iliyopo katika Mji Mkuu wa  Havana, Nchini Cuba
Waziri wa Biashara za Kigeni na Uwekezaji  wa Cuba Bwana Rodrigo
Malmierca Dias akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi Mjini Havana Nchini Cuba wakati wa ziara yake ya
Kiserikali Nchini humo. Nyuma ya Makamu wa Pili wa Rais ni Balozi wa
Tanzania Nchini Cuba Mh. Paul James Makelele

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema upo umuhimu mkubwa wa kuongeza ushirikiano zaidi  kati ya Zanzibar na Jamuhuri ya Cuba hasa katika Sekta ya Biashara na Uwekezaji kwa nia ya kustawisha Uchumi wa Pande hizo mbili.Balozi Seif alitoa wazo hilo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Biashara za Nje na Uwekezaji vitega uchumi wa Jamuhuri ya Cuba Bwana
Rodrigo Malmierca Diaz yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo Mjini Havana Nchini Cuba. Alisema Maendeleo makubwa na  ya haraka yanaweza kupatikana   katika kipindi kifupi iwapo pande hizo mbili zitafikia maamuzi ya pamoja katika  kuzishirikisha  Sekta binafsi kwenye  Mpango huo muhimu wa Uchumi. Alisema Tanzania na Zanzibar kwa ujumla tayari zimeshafungua milango kwa Taasisi Binafsi za Biashara na Uwekezaji kutoka Nje ya Nchi  na kupelekea  hali ya Uchumi
kukua hatua kwa hatua.  Balozi Seif aliishauri Cuba kuitumia fursa hiyo kwa kuzishawishi Taasisi na Makampuni ya Nchi hiyo kuwekeza Tanzania na Zanzibar kwa Ujumla kwa vile maeneo mengi bado yana rasilimali za kutosha katika uwekezaji Vitega Uchumi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameelezea kuvutiwa kwake na Mfumo wa Utalii unaoendelezwa Nchini Cuba ambao umepelekea Nchi hiyo kukusanya Mapato mengi yatokanayo na Sekta hiyo. “ Zipo baadhi ya changamoto ambazo tumeweza kuzishuhudia katika ziara yetu tuliyoifanya kwenye sekta tofauti ambazo zinakukabilini. Lakini hili linaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka kwa kutumia njia ya ushirikiano katika kutatuza changamoto hizo”. Alisisitiza Balozi Seif Ali Iddi katika maelezo yake kwa Ujumbe huo wa Wiashara wa Cuba. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alishauri kuwepo kwa kiunganisho cha mawasiliano kati ya Mji wa Zanzibar, Dar es salaam na Havana katika kuona Sekta ya Biashara inaleta faida kwa pande hizo mbili. Akizungumzia Kilimo Balozi Seif alisema Zanzibar  iko katika juhudi za kuimarisha ukulima wa Umwagiliaji, hivyo Cuba inaweza kusaidia sekta hiyo kwa vile Tayari imeshakuwa na Wahandisi na wataalamu wa kutosha
katika maeneo hayo muhimu. Naye Waziri wa Biashara  za Nje na Uwekezaji Vitega Uchumi Nchini Cuba
Bwana  Rodrigo Malmierca Diaz alisema Nchi hiyo itaendelea kuwapatia Elimu Watanzania katika ule utaratibu wake inaoutumia wa muda mrefu katika kusaidia Mataifa ya Bara la Afrika. Bwana Rodrigo alisema Uongozi wa Wizara yake unakusudia kutayarisha mpango Maalum wa kutafuta Taasisi zitakazosaidia Miradi itakayoanzishwa ambapo alilitolea mfano Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni  { UNESCO } ambalo tayari limeshazisaidia Nchi za  Cuba na Venezuela katika Miradi ya pamoja. Aliishauri Zanzibar na Tanzania kwa jumla kujiandaa kushiriki katika
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yanayotarajiwa kufanyika Nchini humo tarehe 4   hadi 10 Novemba Mwaka huu ili kujijengea uwezo zaidi wauzalishaji. Alisema mualiko rasmi kwa Tanzania wa Ushiriki wa Maonyesho hayoutatolewa hapo baadaye ambapo aliomba   fursa hiyo kutumiwa
vyema.Cuba kutokana na kuwa na vivutio vingi vya kimaumbile imekuwa ikipokea watalii zaidi ya Milioni
mbili kwa mwaka kutoka sehemu mbali mbali Ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog