Thursday

SHUGHULI YA KUTAFUTA MAITI ZANZIBAR


Meli ya Mv SKAGIT ikimalizikia kuzama jana katika eneo la Chumbe Zanzibar


Shughuli ya kutafuta maiti kwenye ajali ya meli iliyozama nchini Zanzibar ilianza mapema jana huku watu takribani miamoja wakiwa bado hawajapatikana baada meli iliyokuwa inaelekea kisiwani Zanziabr kuzama eneo la Chumbe.

Meli hiyo ilitoka Dar Es Salam  kuelekea kisiwani Zanzibar ikiwa imebeba watu miambili tisini.

Hadi kufikia sasa maiti 39 wamepatikana huku watu zaidi ya 150 wakiokolewa.

Msemaji wa polisi nchini Zanzibar aliambia shirika la habari la AFP kuwa kwa sasa kuna hofu ya kutopatikana manusura wowote waliokuwa katika meli hiyo ya MV Skagit

"shughuli ya kuwatafuta manusura na maiti inaendelea lakini kwa sasa ni vigumu kwa kweli kupata manusura." alinukuliwa akisema msemamji huyo wa polisi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog