Friday

BEYONCE KUSHOOT VIDEO YA WIMBO WAKE WA "I WAS HERE" SIKU YA WORLD HUMANITARIAN DAY.





Mwanadadiva mwenye mtoto mmoja muite mama Ivy mke wa mkali wa kwenye ngoma ya Ortis Jay z akiwa na Boss wa Good Music Kanye West mwanamama Beyonce, amejitolea sauti yake iliyobarikiwa kwenye kitu cha maana. Beyonce ametangaza kufanya video ya ngoma ya “I was Here” kwa heshima ya World Humanitarian Day, siku hiyo wakati akiperform watu watakaoonekana ndo itaonekana kwenye video yake hiyo.
 Diva huyo amejiunga na shirika la United Nations & Humanitarian Aid Organization kwa ajili ya kuzindua kampeni ya kusherekea kazi za kujitolea zinazofanywa na watu mbalimbali na kuwapa moyo watu duniani kote kufanya mambo mema kwa watu wengine ambao wako kwenye matatizo. Video itafanywa na kampuni ya Ridley Scott & Associate na madirectors wakali kama Kenzo Digital na Sophie Muller. Kampeni hiyo inalengo la kufikia watu bilioni 1 na ujumbe mmoja wakati wa uzinduzi siku hiyo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog