Friday

STORI KUTOKA KWA RAIS WA BARCELONA KUHUSU LIONEL MESSI



Stori kutoka Sky Sports ninao waamini kwa mastori ya michezo ni kwamba club ya soka ya Barcelona imethibitisha kwamba inaandaa mpango wa kumuongezea Lionel Messi mkataba mwingine mrefu wa kuendelea kuicheza club hiyo.

Sandro Rossell ambae ni rais wa Barca ambayo mashabiki wake wakubwa ni pamoja na Ay na Fid Q amesema japo mkataba wa sasa wa Messi unaisha miaka minne ijayo, mikakati ya kuutengeneza mkataba mpya baada ya 2016 ndio inaanza sasa hivi.

Amesema lazima utakua mkataba tofauti na huu wa sasa, huo mpya utakua mnene zaidi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambae juzi kwenye mechi na Spartak Moscow alifunga magoli mawili kati ya matatu dhidi ya mawili ya Spartak.


Rossell amesema ni muhimu kwa club yake kuendelea kuwa na Messi na wanapanga ratiba ya kufanya mazungumzo na mchezaji huyo ambae toka amejiunga na Barcelona amefunga magoli 186 mpaka sasa.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog