Niliahidi kuweka Video hii ya JB Mpiana na Mule Mule FBI wa FM Academia walipoimba jukwaa moja huko Dubai.
Wimbo ni 48 Hrs Gecoco ambao ulikuwa kwenye Albamu ya JB Mpiana ya Toujou Humble (TH).
Utasikia JB anatambulishwa na alipopewa Mic aliomba
radhi kuwa ye haongei kiingereza ila cha muhimu alisema kuwa alikuwa
mapumzikoni na alikwenda kibiashara, ila anafurahi kuwaona ndugu zake
vijana wakifanya muziki pale, hii ni changamoto kwa wanamuziki
wanachipukia kama hawa. Post hii imewekwa tena kwa heshma kubwa na
taadhima ya Shabiki wangu Papaa Fororo Jema Salim Mandari Le Fimitive Didi Stone na i yaDallas Texas USA Kitokoooo.
Sulutani, Salvatore de la Patria. Papa Chéri, Bin Adam, l’homme qui a mis l’eau dans coco
pichani ni Mule Mule FBI (R) akiwa na JB Mpiana (L ) wakiimba jukwaa moja.
Meneja wa Klabu akimpa JB Mpiana Zawadi.
Mara nyingi tumekuwa tukisikia majigambo ya
wanamuziki wa Congo walioko nchini wakitamba kuwa waliwahi kufanya kazi
na wanamuziki wakubwa wa huko Congo, lakini ni wachache wenye ushahidi
wa hilo binafsi naweza sema sijaona Video ya mwanamuziki aliyeko nchini
anayesema alishawahi kufanya kazi na wanamuziki wakubwa kama JB Mpiana,
Werrason, Koffi Olomide au mwingine yeyote kwangu mimi isipokuwa Mule
Mule FBI Liberko La Loi.
Anaitwa mule Mule FBI Libeko la Loi, binafsi
namkubali sana mwanamuziki huyu wa bendi ya FM Academia, namkubali kwa
kipaji cha uimbaji alicho nacho na uwezo pia na awapo jukwaani aisee
jamaa ahana muchezo na kazi yake. Hii inaweza kuwa ndio chachu ya
mafanikio ambayo anayafikia kimuziki kwa sasa.
Mulemule alikuwa na Bendi ya FM wana Ngwasuma kabla
ya kuelekea Falme za Kiarabu akiwa na baadhi ya wanamuziki wenzie
walipopata mkataba wa kutumbuiza huko.
Wanamuziki aliokwenda nao pamoja naye ni Queen Suzy
ambaye kwa sasa yuko na bendi ya Twanga Pepeta, na Mpiga gitaa wa FM
pia, Pia yumo yule atalaku maarufu wa Defao anaitwa Theo Mbala kama
unakumbuka albamu ya Familie Kikuta ya Defao ndio yeye alighani humo.
Wakiwa huko katika kazi ghafla siku moja aliibuka JB
Mpiana kwenye ukumbi ambao walikuwa wakifanyia kazi na kwa sababu JB
Mpiana ni mtu wa watu basi alitambulishwa na kuamua kupanda jukwaani
kutoa burudani kidogo kwa mashabiki wake ambao walimshangilia sana. JB
Mpiana alipiga wimbo wa 48 Hrs Gecoco ambao unapatikana kwenye albamu
yake ya Toujou Humble (TH), Mashabiki walifurahi sana na yeye alipopewa
mic pamoja na shukrani zake kwa mashabiki aliwsema kuwa alikuwa pale
kwa shughuli zake za kibiashara na mapumziko na alifurahishwa kuona
ndugu zake wako pale wanaganga njaa.
Mashabiki wa mpira wanaamini Mbrazili yeyote kama
hata hajui kucheza mpira basi hata danadana 20 atakupigia ndivyo ilivyo
kwa Congo unapoongelea muziki wapo wengi mnooo.
Katika wengi hao wapo ambao ni zaidi ya wenzao na
ukimuona mwanamuziki amekubalika Congo ujue huyo anauwezo kweli kweli
na si bla bla. JB Mpiana ni mmoja wa wanamuziki wakubwa wa Congo ambao
wanatamba na muziki wao.
Mulemule anasema ile kuimba pembeni ya JB Mpiana
alijiona kama amepata nguvu na ujasiri wa ziada ambao anao mpaka sasa,
alijifunza mambo mawili matatu toka kwa mkongwe huyo.
Kwa sasa Mule mule yuko na FM wana Ngwasuma hapa
jijini Dar Es Salaam baada ya kuondoka bendi aliyojiunga nayo
aliporejea ya Akudo. Mulemule anatamba sana na kibao chake kipya
ambacho kinapendwa sana majukwaani cha Ndoa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.