
Werrason Ngiama Makanda
Papa Cherry Le Suvereee
Werason amekuwa ni mwanamuziki mwenye wafuasi wengi
tangia Wenge BCBG iparanganyike, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na
Digital Congo Werason ameweza kufikia record iliyowekwa na Papa Wemba
miaka ya 70 na 80.
Tangu kuvunjika kwa kundi hili mwaka 1997 Werason
amekuwa hapewi nafasi na JB Mpiana huku wakipumuliana kwa mashabiki na
umaarufu.
Utafiti huo umechapishwa kwenye mtandao maarufu wa
Digital Congo unasema kuwa Werra amejizolea umaarufu si ndani ya Congo
pekee bali hata nje ya Congo. Kadhalika utafiti huo unasema kuwa
Werrason amekuwa akipendwa zaidi na “walala hoi” na hii inatokana na
tabisa yake ya kufanya maonyesho mengi sehemu wanazoishi watu hao huku
JB Mpiana akiwa na mashabiki wengi wenye maisha ya kati na matajiri.
Wenge ambayo iliingia kwa kasi katika ulimwengu wa
burudani kwa staili ya SAPE (société des ambianceurs et des personnes
élégantes) ambayo ilianzishwa na Papa Wenga, lengo la Papa Wemba ikiwa
ni wanamuziki ambao watanashati wanavaa vizuri na kujiweka kwenye
maisha ya juu ikiwa ni pamoja na sehemu wanazoishi, Wanamuziki hawa
walikuwa wanatoka wote eneo lijulikanalo kama Bandalungwa ama Bandal
ambalo ni maarufu kwa maisha ya mjini kama vile Kinondoni ambapo
wajanja wote wanaishi huko, ila baadaye yalipowachanganyia wakahamia
eneo lijulikanalo kama Socimat kama masaki ambapo watu wenye pesa zao wanaishi.
Mwaka 1997 swali kubwa ilikuwa nani anaweza kuikuza
hiyo Spirit ya wana Bandal maana BCBG WENGE walijitambulisha kama
familia moja. lakini baada ya kuparanganyika kila mtu kivyake
waliwagawa mashabiki pia na kujikuta kila upande unaangukia ama kwa JB
Mpiana ama kwa Werasson.
Kwa mujibu wa tafiti hiyo ambayo ilichapwa wiki
iliyopita ndani ya mtandao wa Digital Congo Werasson ameonyesha
kupendwa zaidi wa masela ambao ni wengi huku JB akisemwa kuwalenga
zaidi watu wa Grade B kwenye Show zake. Kiukweli wakurumba hawa wawili
wanaendelea kutawala mashabiki wa muziki wa Congo mbali na vijana wengi
wanaochipukia kwenye muziki huu na ushindani kati yao ndio umekuwa
chachu ya mafanikio ya muziki huu mpaka leo.
Hakuna aliyedhani JB Mpiana na Koffi wangeweza kuja
kuwa marafiki walivyosasa urafiki ambao mashabiki wanasema kuwa urafiki
wa mashaka na unatokana na Koffi kuhama toka kwa Werrason kwenda kwa JB
Mpiana, hilo lilizidi pale Werra alipokataa kwenda kumpa mkono Koffi na
kumuangukia ili uhasama kati yao uishe, Werra alikataa hilo mbele ya
mashabiki wake takribani elfu 20 ambao walimshangilia sana.
Werrason alifanikiwa kupata Kora Award na baadaye
kuchaguliwa kuwa Balozi wa UNICEF na Mjumbe maalumu wa Amani huko Congo
nafasi ambayo anaitumikia bado.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.