Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha
Kilimanaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa Kilimanjaro Music Awards hivi karibuni wamezindua rasmi ziara ya washindi wa tuzo hizi kwa mwaka 2012.
Ziara hizi zitakazofanyika katika mikoa 6 ya Tanzânia
zitahusisha uvumbuzi wa vipaji vichanga vya wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Mikoa itakayohusishwa ni Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya, Mtwara pamoja na Mwanza na kilele
kuwa Dar es Salaam.
Kama alivyokaririwa meneja masoko wa bia hiyo, lengo kuu la ziara hii ni kuwapa
nafasi wasanii chipukizi kushiriki kikamilifu na kuonyesha vipaji vyao kama
mpango wa bia ya Kilimanjaro wa kuzindua vipaji unavyosema.
“Tunataka kuondoa mawazo hasi yaliyopo kwamba Tuzo za
muziki za Kili ni za Dar es Salaam tu. Mwaka huu licha ya kuwapeleka washindi wa
tuzo mikoani tumeamua pia kuzindua vipaji vipya kweye mikoa hiyo kwani
tunaamini kuwa vipaji vya muziki vinapatikana Tanzânia nzima. Vilevile tutawapa
nafasi wasaniii watakaovumbuliwa kuimba na washindi vinara wa tuzo za Kili
ambapo mshindi mmoja wa kila mkoa ataletwa Dar es Salaam kushiriki kwenye
tamasha la mwisho la ziara, na pia kurekodiwa nyimbo moja ya kumwezesha kuanza
safari yake ya muziki.” Alisema George Kavishe meneja masoko wa bia ya Kilimanjaro.
Kwa mkoa wa mwanza ziara hii ilianza kwa kutafuta vipaji vya wasanii chipukizi ambayo ilifanyika tarehe 29 Aprili ambapo majaji walikuwa ni pamoja na Juma Nature, Proffessor Jay na Queen Darleen.
Jana tarehe 5 may KILI AWARDS WINNERS ILIKUWA NAMNA HII.........
Show
ya hapa Mwanza ilifunguliwa na msanii wa taarabu Isha Mashauzi, shangwe
zilikuwa zakutosha kabisa na wapenzi wa burudani ya taarabu walipata
chakula cha ubongo.
Akafuatia msanii aliyechukuwa tuzo ya RnB anajulikana kama Ben Pol
Misago, Hellen & Dullah
Barnaba, Hellen & Sam Misago
Kaka mkubwa ndio aliyekuwa akiangalia ulinzi wa wasanii wote wakiwa salama
Wacheza show wa msanii Diamond
Ikafika zamu ya mtoto wa Zanzibar AT kupanda kwa steji
Ikafika zamu ya msanii mwenye tuzo 3 kupanda kwa steji, hapa namzungumzia Diamond
Mtoto wa Tanga Roma ndio aliyefunga show kwa upande huu wa Mwanza.Kwa mapicha zaidi ingia hapa
BONGO STAR LINK- DJ CHOKA
KATIKA HARAKATI ZA KUSAKA CHIPUKIZI BOMBA HUKO ROCK CITY ILIKWENDAGA POA KIHIVI........................
washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanzawaliojitokeza kwa ajili ya shindano hili na hapa walikuwa wakiendelea kusubiri kuitwa kwa ajili ya usaili
Jaji wa kusaka vipaji vya wasanii wachanga mkoani Mwanza katika ziara ya washindi wa tuzo za KILI 2012 (Juma Nature- wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa washiriki waliohudhuria kwenye tamasha hilo lililofanyika katika ukumbi wa VILLA PARK jijini Mwanza. kutoka kulia ni Profesa J, Queen Darleen, Nature na Henry Mdimu.
Henry Mdimu akitema cheche kwa vijana chipukizi waliokuwa wamejazana Villa tayari kwa tamasha.
Joseph Haule naye hakubaki nyuma, alifunguka kiume kuwasihi ma-underground wakomae kisabuni na kuwaasa waache uoga bali wafanye kilichotakiwa kufanyika.
Hapa ni baadhi ya washiriki wakionesha manjonjo steji huku wakishuhudiwa vyema na majaji wao..
kazi na dawa ndo mtindo wa kisasa..msosi kama kawa. Hapa ni jopo zima la wasaka vipaji wakipata kipooza koo wakati wa mapumziko kabla ya kurudi kwa raundi ya pili |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.