Baada ya stori kuandikwa kwenye
magazeti kwamba Staa Diamond Platnums anadaiwa kumtelekeza baba yake na
hamjali wala hataki kusikia stori zake, hii ndio kauli ya Diamond
kuhusu hiyo ishu.
Amesema “kiukweli ni vitu
ambavyo mimi vimenishangaza sana kwa sababu sijui chochote nakuja kukuta
tu kwenye magazeti, na nisingependa nisikie swala la mzazi wangu kusema
mimi ni mtoto wake sijui nini na nini kwamba mimi nafanya starehe
sihusiki na yeye sio kauli nzuri kiukweli, ina maana ananijua kwamba
mimi ni mwanae baada ya kuwa DIAMOND”
Kwenye line nyingine Diamond
amesema “siku zote kama alijua mimi ni mtoto wake basi angenisomesha na
kunipa elimu nzuri lakini siku zote nilihangaika na Mama yangu mzazi
akanikuza na kunisomesha kwa shida na tabu zote mpaka leo nimekua hivi,
nisingependa kumsikia mtu yeyote anaongea kwamba mimi ni mtoto wake au
yeye ni nani kwa sababu siku zote hawakuonekana, wasitake kuonekana
kipindi cha Maslahi mtu ndio anajifanya anahusika sana na mimi kama
mtoto wake”
“Haya mambo nilianza kuyasema
toka natoa single ya binaadam sikujua hata kama leo ningekuja kuwa na
Prado, makazi au kuwa na haya mafanikio mengine, baba yangu ataendelea
kuwa baba yangu tu ila siwezi kumpa kipaumbele kama ninachompa mama
yangu kwa sababu kama angetaka hilo angenijali toka mapema” – DIAMOND.
Kwa kumalizia, Diamond ambae
mpaka sasa ametumia zaidi ya milioni 69 kujenga Nyumba yake Tegeta Dar
es salaam amesema “mimi nilikua napenda kusoma na nilikua nafanya vizuri
kwenye masomo yangu lakini sikua na uwezo wa kifedha kuendelea kusoma,
mzazi wangu alikua na pesa ina maana angenijua mimi angenisomesha leo
ningekuja kuwa hata mbunge au hata waziri kwa sababu mi najua nina upeo
mkubwa sana wa kielimu na vitu vingine, sasa nimesota na muziki alafu
leo ndio wanajitokeza, SITAKI WANIACHE NA MAMA YANGU MZAZI”
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.