Tuesday

YOTE ALIYOSEMA DULLY SYKES KUHUSU CHUKI ZA WASANII WAKONGWE KWA WASANII WAPYA WENYE MAFANIKIO.

.
Inawezekana ukawa umesikia sikia stori za baadhi ya wasanii wakubwa wa Tanzania kutopenda maendeleo au mafaniko ya wasanii wapya wanaofanya vizuri this time.
Dully Sykes amekua msanii wa kwanza kujitokeza wakati huu na kukemea wasanii wakubwa wenye tabia hizo.
Amesema “Hilo lipo wazi, msanii kama mimi nasikia raha sana vijana kama Diamond, Tunda Man, Mr Blue, Ally Kiba na wengine wakifanya vizuri, kwa hiyo msanii mkubwa kama utakua umeshindwa kufanikisha kile ulichotakiwa kukifanya alafu kijana mdogo akafanya basi mpigie makofi, kama unaona huwezi kufika pale unapotaka basi waachie vijana wafike, tusiwaingilie”
Kuhusu uwepo wa wasanii wakubwa wenye wivu kwa wadogo wenye mafanikio, Dully kasema “Wivu utakuepo unajua huwezi kuona kijana kaanza juzi tu alafu leo anafanya kitu kizuri ukafurahia lakini sijui mimi nina moyo gani tofauti na wenzangu, nafurahia sana vijana wakifanya vizuri kama Diamond, Linah, Amini, Barnaba na wengine wanaofanya vizuri”
Kwenye line nyingine Dully amesisitiza kwa kusema “sioni sababu ya mimi kumchukia mtu, sisi wasanii wakongwe wazee ambao tupo kwenye game siku nyingi, tufurahie kazi ya vijana wanayoifanya tumfurahie Diamond, Barnaba, Amini, Mr Blue na wengine wote, tuwafurahie wale…….. na sio kwamba nimemsema mtu wala kumlenga mtu”

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog