Tuesday

TAARIFA KUHUSU UKIMWI USIOSIKIA DAWA AFRIKA MASHARIKI NDIO HII.


Makao Makuu ya WHO Geneva.
Inawezekana stori nyingine huwa unazichukulia poa, lakini hii usiichukulie poa hata kidogo.
Ninachotaka kukwambia ni kwamba aina ya ugonjwa wa ukimwi ambao hausikii dawa umekua ukiongozeka kwenye hili bara la Afrika katika muda wa muongo mmoja uliopita.
BBC wamesema, kuna ripoti ilimeandikwa na wataalam kwenye jarida la kisayansi la Lancet.
Wataalamu hao wamesema hali hiyo ya ugonjwa kutosikia dawa huenda ikatokea ikiwa wagonjwa hawata zingatia na kutumia dawa walizopewa na pia ufuatiliaji mbaya.
Hali hiyo inazusha hofu zaidi katika bara la Afrika ambako hakuna njia mbadala ya kuwatibu wanaouguwa maradhi ya Ukimwi ambapo watatifi kutoka shirika la Afya duniani-WHO na chuo kikuu London wamegundua kwamba aina ya ukimiwi ambao hausikii dawa unapatikana zaidi kwenye nchi za Afrika Mashariki.
Yani wanasema asilimia 26% ya waathirika wako katika hali hiyo ikilinganishwa na asilimia 14 katika nchi zilizo kusini mwa Afrika, Lakini kwenye nchi za Amerika, Afrika Magharibi na kati hakuna kitu kama hicho.
Chanzo kikubwa cha hayo yote ni kwa sababu wagonjwa hawatumii dawa kama inavyotakiwa ambapo hii stori imetoka siku tano tu baada ya kumsikia waziri mkuu Mizengo Pinda akisema Tanzania imekua miongoni mwa nchi 36 duniani zilizofanikiwa kupunguza maambukizi mapya ya UKIMWI kwa asilimia 25.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog