Saturday

HUYU NDIO RAPPER ALIEMCHANA RICK ROSS KWA VIDEO ALIYOIFANYA NIGERIA.

.
Ni siku chache zimepita toka rapper Rick Ross kutoa video ya ‘hold me back’ aliyoishoot Nigeria ambapo ndani yake kumeonyeshwa maisha mabovu wanayoishi Wanigeria.
Ni video ambayo hata kwenye mitandao ya kijamii asilimia kubwa ya waafrika hasa Wanigeria wameiponda na moja kati ya mambo ambayo yamewaudhi ni kitendo cha Rick Ross kuonekana akiwapa watoto dola za kimarekani.
Rapper M.I amekua staa wa Nigeria wa kwanza kujitokeza na kuiponda hiyo video kwamba mgeni kama Rick Ross hajui chochote kuhusu historia na maisha ya Wanigeria, ameivalisha nchi picha mbaya.
Kwenye line nyingine M.I amesema huko ni kuivunjia nchi heshima ndio maana hajaifurahia kabisa hiyo video na isitoshe Rick Ross alikua na uwezo wa kuonyesha maeneo mengine na siyo hizo picha mbaya tu.
Kama hujapata nafasi ya kuichek hiyo video ya Rick Ross ichek hapo chini.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog