Fukuza fukuza ya klabu ya Yanga
iliyoanza baada ya mkutano wa wajumbe wa kamati ya utendaji uliofanyika
makao makuu ya klabu imeendelea na imemkumba kocha mkuu wa klabu hiyo
Mbelgiji Tom Saintfiet.
Taarifa za uhakika kutoka kwa
makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga ni kwamba uongozi wa timu
hiyo umefikia maamuzi ya kumtimua kazi kocha huyo aliyeajiriwa miezi
mitatu iliyopita kutokana na kutofautiana sera za namna ya kuiendesha
klabu na uongozi wa juu wa mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati.
kamati ya utendaji
ilisimamisha ajira za viongozi waajiriwa wote wa klabu hiyo akiwemo
katibu mkuu Celestine Mwesigwa na msemaji Luis Sendeu huku ikitoa onyo
kwa kocha Saintfiet kwa tabia yake ya kuongea na waandishi wa habari
bila mpangilio wa klabu lakini baada ya taarifa hizo kutoka usiku wa
kuamkia leo kocha huyo akaonekana akiongea kwenye television mojawapo
nchini akizungumzia mambo mbalimbali kuihusu Yanga.
Kwa mujibu wa Sanga anasema kwamba sakata lote la jinsi kocha huyo alivyopoteza kazi yake litatolewa ufafanuzi.
Wakati huo huo aliyekuwa
katibu mkuu wa Yanga kabla ya Mwesigwa, Lawrence Mwalusako amepewa
jukumu la kukaimu nafasi hiyo ya ukatibu mkuu wa Yanga kwa muda wakati
mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Seikolojo Chambua akikabidhiwa majukumu
ya kuwa meneja wa timu hiyo akichukua nafasi ya Hafidh Salehe ambaye
nae aliondolewa.
Nafasi ya usemaji wa Yanga
mpaka sasa imekuwa kitendawili, tetesi zinasema kuwa mtangazaji wa
Clouds FM NA Clouds TV Abdul Mohamed na Mwanahabari Mahmoud Zubeiry
mmojawapo anaweza kula shavu la kumrithi Sendeu.
Stori imeandikwa na shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.