Tuesday

ROMA AFUNIKA TAMASHA LA WASHINDI WA KILI MBEYA

On Streets Today
Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza shoo wake wakati wa onyesho maalum la Washindi wa Kili Music Awards jijini Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine juzi. (Picha: Mpigapicha Wetu)

Nyota wa hip hop nchini, Roma Mkatoliki, aliacha gumzo mjini Mbeya wakati alipofanya shoo ya uhakika na kuamsha shangwe mpya, licha ya kuwa msanii wa pili kutoka mwisho katika ratiba ya watumbuizaji wa onyesho la ziara ya washindi wa tuzo za Kilimanjaro kwenye Uwanja wa Sokoine juzi.
Mashabiki waliimba jina lake tangu msanii huyo alipoitwa stejini na alipofika hakuwaangusha.
Alitumbuiza kwa nyimbo zake kali na wakati mashabiki wakidhani kwamba shoo yake imefikia tamati, rapa huyo alisema: "Sasa ndugu zangu, nawaambia ukweli kwamba kufikia muda huu mmetumia Sh. 200 tu ya kiingilio chenu... sasa nawapa shoo ya Sh. 1,800 iliyobaki.”
Huku mashabiki wakishangilia kwa nguvu, Roma alimalizia kwa kuimba wimbo wa Mathematic uliompa tuzo.
Wasanii wengine waliopanda stejini ni pamoja na Ben Pol, AT, Ali Kiba, Barnaba, Ommy Dimpoz na Suma Lee ambao nao walifanya shoo ya uhakika.
Mshindi wa tuzo ya wimbo bora wa R&B, Ben Paul ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia wimbo wake wa 'Number One', alifungua jukwaa na kuwaamsha watu kuwa sasa shoo imeanza.
Alifuata jukwaani Suma Lee ambaye aliongozwa na shoo kali kutoka kwa vijana wake wanne wa kike na wa kiume na kushangiliwa vilivyo.
Kisha alipanda mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili, Ally Tall a.k.a AT na kutoa burudani ya nguvu na wimbo wa 'Vifuu Tundu' akiwa na wanenguaji wake wawili wa kike.
Nyota wa wimbo 'Baadaye', Ommy Dimpoz alipanda jukwaani na kutumbuiza kwa wimbo huo pamoja na 'Nai Nai' uliompa tuzo ya Wimbo Bora wa Kushirikiana aliomshirikisha Ali Kiba.
Ali Kiba alibaki jukwaani hapo kama ilivyokuwa mjini Moshi na vijana wake kumfuata kutoa shukrani zao za kupata kura zilizowapa ushindi wa tuzo ya Wimbo Bora wa Zouk Rhumba kupitia wimbo wa 'Dushelele'.
Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume, Barnaba ndiye aliyefunga pazia hilo mjini Mbeya kwa kuimba wimbo wake unaotamba sasa wa 'Magube Gube'.
Wasanii hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo jijini Mjini Mtwara, baada ya kuwa tayari walishatumbuizakatika miji ya Dodoma, Mwanza na Moshi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog