Wednesday

ATC YAPATA NDEGE MBADALA: HILI NALO LINAHITAJI KEKI NA MASHADA YA MAUA?

Yapo mambo ambayo hata unapotaka kuyakalia kimya tu inakuwa shida kidogo.Juzi,Shirika La Ndege Tanzania(ATC) limepata ndege mbadala(nasema mbadala badala ya mpya kwa makusudi).Ndege hii imekodishwa...Je ni kweli kuwa Uwezo wa kununua bado hatuna?.Cha kusikitisha zaidi ni kwamba tunavishana mataji kujipongeza kwa kufanikiwa kukodi ndege moja ya abiria!!!!????
Pamoja na hayo,kwetu sisi yaelekea kuwa na ndege ya kukodisha ni mafanikio makubwa sana.Yanastahili makofi,vigelegele na keki.Kweli??
 
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakishuka katika ndege mpya aina ya Boeing 737-500 iliyokodishwa na shirika hilo yenye uwezo wa kubeba abiria 108. Ndege hiyo itaanza kuruka baada ya wiki moja.
 
Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi akiongea na waandishi wa habari mara bada ya kuwasili kwa ndege mpya aina ya Boeing 737-500 iliyokodishwa na shirika hilo yenye uwezo wa kubeba abiria 108.
 
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikata keki kusherekea ujio wa ndege ndege mpya aina ya Boeing 737-500. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL ) Paul Chizi
GOD SAVE US!
Picha na maelezo ya picha kwa hisani ya G.Sengo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog