Tuesday

KUHUSU MGOGORO WA MPAKA NA MALAWI, HII NDIO KAULI MPYA YA TANZANIA.

Straight kutoka bungeni Dodoma kuhusu ishu ya mpaka wa Malawi na Tanzania ni kwamba waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe amesema Malawi wanadai kwamba mpaka wa Tanzania na wao kwenye ziwa Nyasa unapita Pwani hivyo ziwa lote kutoka kwenye mpaka wa Malawi na Mozambique hadi Kyela ni mali ya Malawi.

Amesema “serikali yetu ilipata habari za kuaminika kupitia shirika la TPDC kuwa eneo lote la ziwa Nyasa kaskazini mwa Msumbiji limegawanywa kwenye vitalu na kwamba serikali ya Malawi imevitoa vitalu hivyo kwa kampuni ya utafiti wa mafuta na gesi”

“Makampuni hayo yaliomba kibali cha kuruhusu ndege za utafiti ziwani humu ombi ambalo jeshi la Wananchi wa Tanzania lilikataa, pamoja na katazo hilo serikali yetu ilipata ushahidi kwamba ndege ndogo za utafiti zenye uwezo wa kutua majini na ufukweni zinazokadiriwa kuwa tano zilionekana zikivinjari na kutua katika ziwa Nyasa upande wa Tanzania na kwenye ufukwe wake January 29 na July 2 2012″ – Bernard Membe

“Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inathamini sana uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi mbili na ina dhamira ya kudumisha na kuimarisha uhusiano wa ujirani mwema kwa manufaa ya watu wetu, inapenda kuchukua nafasi hii tena kuitaka serikali ya Malawi kuheshimu makubaliano ya July 27 2012″ – Waziri Membe.

Pamoja na ahadi ya kuwalinda raia laki sita waliopo kwenye mwambao wa ziwa Nyasa, Waziri Membe amesema “serikali ya Tanzania inapenda kuchukua nafasi hii tena kuyaonya na kuyataka makampuni yote yanayofanya shughuli ya utafiti kwenye eneo hilo kusitisha kuanzia sasa, kuacha shughuli za utafiti katika maeneo hayo”

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Search This Blog